Wasanii
kadhaa wa dancehall na reggae kutoka nchi ya Jamaica wameratibiwa kutumbuiza
nchini Kenya hivi karibuni.
Takriban
wasanii sita tayari wametangaza kuwa na matamasha nchini kuanzia mwezi ujao na
mwaka kesho.
Christopher Martin ndiye mwimbaji wa hivi punde zaidi kutangaza kuwa atakuwa nchini kwa tamasha. Mtunzi huyo wa kibao 'Cheaters Prayer' mnamo Jumatatu alitangaza kwamba atatumbuiza nchini mnamo Februari 8, 2025.
“Hatimaye Kenya!!! Imekuwa muda mrefu na nimefurahi sana tutaungana tena hivi karibuni !!,"
Christopher Martin alitangaza kupitia mitandao yake ya kijamii.
"Tuonane tarehe 8 Februari 2025 katika bustani ya Uhuru kwa ajili ya @SoundsfromAfrica.Fest," aliongeza.
Wasanii wengine watakaotumbuiza nchini hivi karibuni ni pamoja na;
o Sean Paul – mwimbaji dancehall na r&b (Desemba 1, 2024)
o Etana – mwimbaji reggea na dancehall (Desemba 7, 2024)
o Shenseea – mimbaji dancehall (Desemba 13, 2024)
o Christopher Martins – ukumbi wa reggae na densi (Februari 8, 2025)
o Dexta Daps – mimbaji dancehall (tarehe isiyothibitishwa hivi karibuni)
o Vybz Kartel – mimbaji dancehall (tarehe isiyothibitishwa mwaka wa 2025)
Wasanii
wengine kadhaa wa Jamaica tayari wametumbuiza nchini humo mwaka huu. Wasanii
hao ni pamoja na Burning Spear, Glen Washington, Konshens, Kranium, na
Turbulence.