Mtangazaji wa redio Jambo Gidi amemwomboleza mchezaji wa mpira wa wavu Janet Wanja Mungai kwa kuchapisha picha na video ambazo amesema kwamba zilipigwa miezi michache iliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram @gidiogidi , mtangazaji huyo wa kipindi cha asubuhi redioni cha Gidi Na Ghost asubuhi, katika ujumbe wake amesema kuwa video na picha alizochapisha zilirekodiwa takribani miezi minne iliyopita katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika nchini Ufaransa.
“Hizi nii picha za mwisho na video nilizorekodi nikiwa na Janet Wanja miezi minne iliyopita katika Olimpiki ya Paris. Haya maisha hayatabiriki tu.” Aliandika Gidi.
Kwenye ujumbe wake, Gidi amenukuu maneno ambayo Janet Wanja alimweleza wakati walikuwa wanasakata densi aina ya isukuti kwenye burudani la Wakenya katika sherehe hizo wakati wa Olimpiki.
“Gidi wacha tudance na Marie-Rose yawa.” Gidi alinukuu maneno aliyoyasema Janet Wanja miezi mine iliyopita.
Mtangazaji huyo aidha amesikitikia kifo cha mchezaji huyo wa voliboli akisema kuwa Janet Wanja alikuwa mtu mwenye roho ya ukarimu daima atamkumbuka kupitia video aliyorekodi nchini Ufaransa.
“Tumempoteza mwanamichezo wa haiba aliyekuwa na roho ya wema. Daima
nitakukumbuka katika densi hii na binti wangu. Pumzika kwa amani ya milele.”
Aliandika mtangazaji Gidi kwenye anwani
yake ya Instagram.
Janet Wanja aliaga dunia Alhamisi kutokana na
saratani ya nyongo.