Bosi huyo wa Wasafi amesisitiza kwamba anamjua Muumba wake, Mwenyezi Mungu na yuko tayari kutenda mema ya kumpendeza.
Mwanamuziki huyo akizungumza ameweka wazi kwamba baadhi ya watu wanamuona kama mkatili na kumuuliza mbona aswali na anaimba. Ameweka wazi kwamba iwapo anatania basi mwenyewzi Mungu ndie anajua hilo.
"Mimi namuomba mwenyezi Mungu na nahakikisha kwamba nafanya mambo mazuri. Sishituki sijali wala siogopi kumtumikia mtu. Umuhimu kwangu ni kuhakikisha kwamba nimepata nafasi, na mimi nafasi hii ni ya kuwasaidia watu. Mwenyezi Mungu kanibariki na mimi vilevile nabariki wengine," Diamond alisema.
"Kama ni kuhusu kufuturisha, nitafuturisha, kama ni kuhusu kutoa sadaka ndivyo hivyo nafanya,' aliongeza mwanamuziki huyo.
Kiongozi huyo wa Wasafi ameongeza na kusema kwamba wakati unapoaamua kufanya jambo, maneno ya watu yasikufanye ukate tamaa. Akizungumza ameweka wazi kwamba yeye anafanya maamuzi yake kwa sababu ya mwenyezi Mungu na kwa hivyo maoni ya watu sio tishio kwake.
"Maoni ya watu huwezi kuyaepuka. Kila mtu atatoa maoni yake kama anavyoona yeye. Kama unafanya kwa sababu ya watu utaogopa maoni ya watu. Lakini mimi nafanya kwa sababu ya Alah kwa hivyo comment yangu nitaikuta kwa Alah ikitokea siku nikifa. Hicho ndo kitu ninachokiangalia," aliweka wazi msanii huyo.
"Fanya mambo mazuri na ukitaka watu wajue unafanya mambo mazuri usikatishwe tamaa. Mungu anasema msikate tamaa na neema zangu. Mwenyezi Mungu ndio anaelekeza hilo kwamba isitokee kiumbe cha kukukatisha tamaa, fanya mambo mazuri," alisisitiza.
Akizungumza amewataka wanaochagua kutenda mema kutokubaliana na maoni ya watu na badala yake kuwa tayari kuendelea na juhudi za maamuzi yao.
Haijalishi unafanya kazi gani , unafanysa kitu gani, hakikisha unaswali. Mimi naswali maraa tano kwa siku, sasa hivi nina mika mitatu.
Utasikiza mtu wa watu anakwambia, unaimba alafu unaswali unafiki, unafiki wangu anaujua mwenyezi Mungu. Nafunga naswali pia," aliweka wazi