Jay ameweka wazi kwamba 'bifu' ilikuweko kwa muda mrefu sana jambo ambalo liliweka uandui mkubwa miongoni mwa nchi hizo mbili za Afrika mashariki hasa kwenye tasnia ya muziki.
Msani huyo wa zamani Tanzania ameeleza kwamba mwenzake wa Uganda alimuibia wimbo wake bila idhini yake jambo ambalo lilimkwaza sana na kumkosesha amani.
"Mwanzo nilipofika Uganda nikakutana na Jose Chameleon na tukazungumza vizuri na tukaunda urafiki, alipokuwa akija Tanzania ananitafuta. Mwaka 2005 nilitengeneza wimbo 'Nikusaidiaje' alipenda ile biti na akaichukua. Baadaye nikaja kumuuliza kwa nini amechukua wimbo wangu bila idhini yangu? Ikaja utata na kukawa na bifu nzito sana," aliweka wazi Profesa Jay.
"Mimi na Chameleon tukawa na uwadui mkubwa sana. Ile bifu illikaribia ya Idd Amin na Nyerere. Chamelion msanii mkubwa sana Uganda nami mkubwa Tanzania. Lakini niliumizwa na yeye kutumia wimbo wangu na yeye ni mshikaji wangu kwa nini asingeniambia," aliendelea zaidi.
Mwanamuziki huyo ameeleza kwamba alikuwa anakerwa mara kwa mara kila nchi aliyozuru alikua anaulizwa mahali ugomvi wao umefikia wapi, jambo amblo lilimfanya kuondoa nyongo ili kuondoa uadui miongoni mwao.
Niliona hiyo bifu inaenda mbali na ingefanya ichi zetu ziingie kwenye uadui. Nilialikwa kwenda uganda kwenye tuzo fulani, Chameleon aliposikia niko Uganda akanialika nyumbani kwake. Nilipoenda akaniambia yuko radhi kwa kilichotokea. Wakati huo ili kuiondoa uadui uliokuwepo ikabidi tutengeneze ngoma na tukaingia kwenye studio yake na tukatengeneza wimbo "Ndivyo Sivyo," alieleza Zaidi msanii huyo wa bongo.
"Watu wengi hawakutarajia kwamba uadui wetu utakuja kukamilika maana ulikuwa umefika mbali,"
Akizungumza kwenye kikao na wanahabari pia ameeleza changamoto ambazo walikumbana nazo kama wasanii wa zamani tofauti sana na wasani wa sasa wa kizazi kipya.
"Tulikuwa tunafanya mziki ki analog, ilikuwa mkifanya mziki ata mkiwa watano mnajipanga kwenye microphone, anaanza wa kwanza, wa pili, akikosea wa tano mnaanza upya. Sasa hivi mziki umebadilika. ninaweza nikatengeneza verse yangu hapa situdio nikamutumia Khaligraph Jones uko Kenya akaingiza verse yake kisha atume data nitengeneze na iwe kolabo," alieleza