Katika kitengo cha Dunia na unafiki ni Pacha niliazimia kuangazia makala ya msanii mmoja kutoka Tanzania aliyeitwa Wabiro Wakazi.
Kwenye chapisho lake katika mitandao ya Kijamii instagramu Bwana wakazi alielezea kuwa ipo kasumba kali na tabia za kinafiki ambazo binadamu wamekuwa nazo kwa miaka mingi ambazo si nzuri.
Alisema kuwa kwa mara si haba watu mara nyingi wameonekana kutowathamini watu wengine na badala yake wamekuwa wakifatilia maisha ya watu wengine kwa karibu huku wakiwasimanga kwa mabaya.
Alisema kuwa kwa mara si haba uadilifu ndani ya watu umewatoka kwa kiwango kikubwa sana na kurai kuwa ni lazima tujirudi .
Alisema kuwa siku hizi si kama zama za kale ambapo watu walikuwa wakiwasifia wengine kwa kutekeleza mambo mema na badala yake siku hizi mtu aonapo mtu anapiga hatua ya maendeleo yeye huanza kwa kumchimba mizizi na kutaka kujua ni wapi alikopata pesa za ujenzi.
Alisisitiza kuwa mtu anapopata fursa ya kuinuka kati ya watu wengine anastahiki kupewa pongezi na heko kwa kazi murwa tena yenye tija kwa kufanya hivyo anajenga uhusianpo na hamasa miongoni mwa watu walio na idili ya kufanikiwa kama yeye.
Hata hivyo katika kauli sambamba na usemi wa bwana Wakazi niliweza kupiga tathimini yake na kubaini fika kuwa binadamu siku zote ni nduma kuwili huwa hataki ufanisi kwa vyovyote vile.