UZINDUZI WA BANDARI YA LAMU

Mwanaume mmoja akamatwa kwa kusababisha taharuki Lamu

Labda uliona video ya rais Kenyatta akionekana kushtuka wakati alipokuwa anapeana hotuba. Je, ni kipi kilichotokea?

Muhtasari

•Kinyua alikamatwa baada ya kusababisha hali ya taharuki wakati rais anatoa hotuba

•Alisema kuwa alitaka kutoa lalamishi kuhusu ugavi wa kazi katika eneo hilo.

sherehe ya kuzindua bandari ya Lamu
sherehe ya kuzindua bandari ya Lamu
Image: Hisani

Labda uliona video ya rais Kenyatta akionekana kushtuka wakati alipokuwa anapeana hotuba. Je, ni kipi kilichotokea?

Mwanaume mwenye umri wa wastani alikamatwa siku ya Alhamisi baada ya kujaribu kulamisha kumfikia rais Kenyatta alipokuwa anatoa hotuba katika sherehe ya kufungua bandari la Lamu.

James Kinyua Wamuchomba ambaye alidai kuwa alitaka kutoa lalamishi la kutoridhika na ugavi wa kazi kwa wenyeji wa eneo hilo anatarajiwa kufikishwa kotini siku ya Alhamisi.

Kinyua alikuwa baadhi ya waliokuwa wamealikwa. Aliwapita maafisa wa ulinzi ila akazuiwa akiwa amefika futi kidogo tu kumfikia rais wakati mmoja wa wasaidizi wake rais alipomuona na kujulisha maafisa.

Rais alimuona Kinyua akikaribia na kuonekana kushtuka ghafla ila maafisa walimshika alipokuwa anapiga kelele kwake rais.

Pole sana ni mtu tu na mambo yake” rais alisikika kusema baada ya tukio hilo.

Baada ya kukamatwa, Kinyua ambaye alikuwa ameshikilia kitambulisho chake tu alihojiwa ndipo akasema kuwa alitaka kutoa lalamishi kuhusu ugavi wa kazi katika eneo hilo.

“Alikuwa amejihami na kitambulisho tu kwa hivyo hatudhani alikuwa na lengo la chinichini. Hata hivyo, atashtakiwa pamoja na wengine kwa kusababisha usumbufu” Alisema afisa mmoja mkuu.