UHALIFU KAKAMEGA

Majambazi watano wapigwa risasi Kakamega

Bunduki mbili na mavazi ya polisi ni baadhi ya vitu vilivyopatikana kwenye tukio hilo

Muhtasari

•Watano hao walikataa kutii amri ya kusimama na wakaanza kupiga risasi

•Bunduki mbili na mavazi ya polisi ni baadhi ya vitu vilivyopatikana kwenye tukio hilo

Crime scene
Crime scene

Majambazi watano waliuliwa kwa kupigwa risasi alasiri ya Jumanne katika eneo la Makhokho lilio kwenye barabara ya  Kakamega-Kisumu.

Watano wale walikabiliwa na maafisa wa huduma maalum(SSP) walipokuwa wanatoka kwenye shughuli yao ya wizi wa kimabavu mjini Kakamega.

Maafisa wa SSP walilazimishwa kutumia bunduki zao baada ya watano wale waliokuwa wanasafiri kwa gari ndogo aina ya Toyota Belta kupuuza amri ya kusimama na kisha kuanza kupiga marisasi kuelekeza upande waliokuwa maafisa wale.

Hata hivyo, mashambulio ya majambazi wale waliokuwa wamejihami kabisa hayafua dafu kwani maafisa wa SSP waliwapiku nguvu na kuwaacha katika hali mahututi.

Shirika la kuchunguza uhalifu(DCI) lilitangaza kuwa watano wale walikuwa wanapanga njama ya kutekelea uhalifu mjini Bungoma na Mumias.

Bunduki mbili zilizokuwa na risasi, simu ya polisi na mavazi ya polisi ni baadhi ya bidhaa zilizopatikana na majambazi wale.

Bidhaa zilizopatikana
Bidhaa zilizopatikana
Image: HISANI

Hakuna yeyote kati yao aliyenusurika huku miili yao ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kakamega County Referral Hospital.