BBI: Mahakama kuu yakubali ombi la dharura la Kihara

Jopo la majaji watano limedhibitisha wasilisho la mwanasheria mkuu la kusitisha maamuzi dhidi ya BBI kuwa la dharura

Muhtasari

•Mwanasheria mkuu Kihara Kariuki alitaka mahakama kusitisha kwa muda utekelezwaji wa  maamuzi yaliyotolewa dhidi ya mchakato wa BBI

• Mahakama imeamuru kuwa wasilisho hilo linafaa kushughulikiwa kwa dharura huku ikielekeza wahusika kuwasilisha mawasilisho yaliyoandikwa kabla ya mwisho wa siku ya Alhamisi

kihara Kariuki
Image: maktaba

Mahakama kuu imeidhinisha kuwa dharura ombi la kusitisha kwa muda utekelezwaji wa maagizo ya mahakama kuu dhidi ya mchakato wa BBI yaliotolewa siku ya Alhamisi.

Jopo la majaji watano lilidhibisha kuwa ombi liliwasilishwa na mwanasheria mkuu Kihara Kariuki la kuitaka mahakama  linafaa kushughulikiwa kwa dharura huku likielekeza wahusika kuwasilisha mawasilisho yaliyoandikwa kabla ya kufungwa kwa shughuli za siku ya Alhamisi.

Mahakama ilisema kuwa ingeamuru kulingana na mawasilisho yatakayokuwa yamewasilishwa kwa barua pepe siku ya Jumatano tarehe wiki ijayo.

Kihara alitaka jopo mahakama kusimamisha amri iliyotolewa wiki iliyopita ili aweze kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.