logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Video: Pasta Mackenzie awaomba wanahabari kumnunulia mkate na maziwa

Katika hali ya kuchekesha, Mackenzie alisema kuwa yeye yuko ndani na amefungiwa bila pesa.

image
na Davis Ojiambo

Habari05 June 2023 - 08:13

Muhtasari


  • • Mchungaji huyo aliyeonekana kuzungumza kwa ucheshi aliwaambia wanahabari kwamba ni wajibu wao kumpa mkate na maziwa kwa sababu maudhui yake yamewaingizia kipato kikubwa.
Mackenzie aomba mkate na maziwa kutoka kwa wanahabari.

Mhubiri tata Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International amewashangaza wanahabari baada ya kuwataka kumnunulia mkate na maziwa angalau kama njia moja ya kurudisha shukrani kutokana na kile alisema kuwa wamepata hela ndefu sana kutokana na kuangazia taarifa na habari zake na msitu wa Shakahola.

Mackenzie ambaye aliwasilishwa mahakamani siku ya Ijumaa baada ya kuwa rumande kwa siku 30 anakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwemo ya mauaji ya halaiki ambao walifariki na kuzikwa katika makaburi ya jumla huko Shakahola baada ya kusemekana kuwa Mackenzie alikuwa anawarai kujinyima chakula na maji ili kumuona Mungu.

Kaitka ombi lake kwa wanahabari, Mackenzie alisema kuwa amefungiwa na hana uhuru wa kujipatia pesa na hivyo ingekuwa jambo la busara kwa wanahabari hao kumnunulia mkate na maziwa.

“Mmeunda pesa nyingi sana lakini hamwezi ninunulia hata mkate. Mimi nimekaziwa siwezi kupata hata pesa. Si mwende mniletee angalau na pakiti ya maziwa bana. Angalau bana mimi niko ndani wewe uko nje, ama namna gani bwana,” Mackenzie aliwaambia wanahabari hao katika klipu ya video ambayo imeibuliwa.

Itakumbukwa kuwa mchungaji huyo mwenye utata anaandamwa na tuhuma za kuwarai waumini wake kujitesa njaa ya maji na chakula hadi kufa katika kile alikuwa anawaaminisha kuwa ndio njia pekee na sahihi ya kukutana na Mungu.

Kufikia sasa, Zaidi ya maiti 240 zimefukuliwa katika shamba la Shakahola lenye upana wa ekari 800 na wikendi iliyopita akiongea katika ibada ya kanisa huko Kirinyaga, waziri wa usalama wa ndani profesa Kithure Kindiki alisema kuwa awamu ya tatu ya kufukua maiti kwenye shamba hilo itang’oa nanga Leo Jumatatu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved