logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakenya wazungumzia baridi iliyotanda jijini Nairobi

Wakenya waelezea kuhusu baridi ambayo imeongezeka hii leo Alhamisi Julai 18,2024.

image
na Davis Ojiambo

Habari18 July 2024 - 08:41

Muhtasari


  • •Mtayarishaji wa maudhui Azziad Nasenya kupitia ukurasa wa Instagram aliandika;"Hii baridi ya leo iko na PHD juu wueeh"
  • •Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya ilionya wakenya kujiandaa kutokana  na mvua kubwa zaidi mnamo Julai ambayo inaweza kugeuka kuwa mvua ya mawe mnamo Agosti.

Baadhi ya wakenya wameibua wasiwasi kuhusu baridi ambayo imeenea kote jijini Nairobi hii leo Alhamisi Julai 18,2024.

Mwanatiktok na mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali, Azziad Nasenya kupitia ukurasa wa Instagram aliandika;

"Hii baridi ya leo iko na PHD juu wueeh"

Kwa upande mwingine mwanahabari wa runinga ya Citizen Stephen Letoo ,kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika;

"Watu wa Nairobi hii ni baridi ama ni fridge...?"

siku ya Jumapili, Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya ilionya wakenya kujiandaa kutokana  na mvua kubwa zaidi mwezi Julai ambayo inaweza kugeuka kuwa mvua ya mawe mnamo Agosti.

Idara hiyo ilieleza kuwa mvua ya Julai sio ya kawaida na kwamba ilisababishwa na mwingiliano wa hewa baridi kutoka mashariki na hewa ya joto kutoka magharibi.

"Si ajabu kupata mvua mwezi Julai nchini Kenya. Hii hutokea wakati hewa baridi kutoka mikoa ya kati na mashariki, ikiwa ni pamoja na Nairobi, inapoingiliana na hewa yenye unyevunyevu kutoka magharibi."

"Hewa yenye uvuguvugu hupanda juu ya hewa baridi, na kusababisha mvua kubwa," idara hio ilieleza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved