KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Julai 28.
Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Trans Nzoia, Siaya na Kakamega.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya ICD na Mombasa Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya JKUAT, Juja, na Kenyatta Road zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za mji wa Kitale, Kisawai na Saboti katika kaunti ya Trans Nzoia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Luanda Kotieno, Kitambo, na Chianda katika kaunti ya Siaya pia zitaathirika.
Sehemu za mji wa Kakamega, State Lodge na MMUST katika kaunti ya Kakamega pia zitakosa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.