
Muda mchache baada ya kuachiliwa bila mashtaka, mwanaharakati
wa haki za kibinadamu Boniface Mwangi amesema kuwa waziri wa maswala ya ndani
Kithure Kindiki hafai kushikilia nafasi katika ofisi ya umma.
Kupitia mtandao wake wa X, Mwangi amesema kwamba wakenya wengi wametekwa nyara na wengine kuulliwa kwa njia zisizoeleweka chini ya utawala wake kama CS wa usalama.
Kulingana na mwanaharakati huyo, hatua ya rais Dkt. William
Ruto kumpandisha hadhi Kithure Kindiki kuwa naibu wa rais wa taifa la Kenya ni
kuzidisha uhuru wa kiongozi huyo na uasi wa sheria.
“Chini ya uongozi wake, wananchi wametekwa nyara na kuuwawa
na kumekuwa na ongezeko la kushangaza la mauaji ya wanawake.” Aliandika Mwangi.
Vile vile, mwanaharakati huyo ameitaka serikali kuzifidia
familia ambazo zilipoteza wapendwa wao waliouliwa na polisi katika maandamano
ya mwezi Juni ya kupinga mswada wa fedha.
Mwanaharakati huyo aliwachiliwa huru Jumatatu asubuhi baada
ya kukesha katika kituo cha polisi cha Kamukunji.
Mwangi alikuwa amekamatwa Jumapili asunuhi nyumbani kwake
Courage Base katika eneo la Ukambani kwa madai ya kuchochea wananchi kuandaa
maandamano katika hafla ya mbio za Standard Chartered marathon zilizofanyika Jumapili jijini
Nairobi.