RAIS WILLIAM RUTO alizua vichekesho Alhamisi wakati wa uzinduzi wa chuo cha mafunzo ya uuguzi cha Kerio Valley katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Rais alikuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi
walioandamana naye katika ziara yake ya bonde la Ufa iliyong’oa nanga hiyo
Alhamisi alipomtania mbunge wa Kapsereti Oscar Sudi kuhusu kutambulishwa kwake
kama ‘mhandisi’.
Baada ya kuwatambulisha viongozi wengine wengi, Ruto
alionekana kumsahau Oscar Sudi ambaye ilibidi watu kupiga kelele kumjulisha
rais uwepo wa mbunge huyo mkwasi.
“Ooh,
tuko na huyu injinia. Sijui ni injinia wa nini lakini tu ni injinia tusema,
anaitwa Oscar Sudi. Nasikia zamani alikuwa area huku sasa amepelea uinjinia
mpaka umefika Eldoret. Ahsante sana,” Ruto alisema
akimtambulisha Sudi kwa umma kwa njia ya utani.
Kitembo cha Sudi katika Nyanja ya masomo kimekuwa ni
mjadala pevu kwa miaka mingi sasa humu nchini.
Mbunge huyo ambaye ni mtetezi mkali wa sera za rais
William Ruto alijipata kuwa gumzo la mitandaoni mwaka jana baada ya kufichua
kuzawadiwa shahada na chuo kimoja.
Sudi alifichua kwamba alivishwa joho na shahada ya
uzamili ya kiheshima na chuo cha Northeastern Christian wakati alipoudhuria
hafla ya kufuzu kwa mahafali katika chuo anuwai cha Eldoret.
Shahada hiyo ilivutia joto la kisiasi kutoka kwa
baadhi ya watu, hadi ikapelekea mamlaka inayosimamia elimu ya juu CUE kuingilia
kati na kutaka shahada hiyo kuchunguzwa na kufutiliwa mbali ikiwezekana.