logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dkt Fred Matiang’i arejea nchini kujiweka tayari kwa kampeni za urais wa 2027

Matiang’i anatarajiwa kuungana na wapinzani wengine wa serikali akiwemo Kalonzo, Gachagua, Wamalwa, Karu na Kebaso kwa lengo la kutwaa ushindi 2027.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari18 April 2025 - 11:12

Muhtasari


  • Kioni, haswa, amesisitiza mara kwa mara Matiangi kuongoza chama katika kinyang'anyiro kifuatacho cha uchaguzi.
  • Pia alionya dhidi ya majaribio ya kukwamisha azma ya Matiangi ya kisiasa, akisisitiza kuwa juhudi zozote za kumzuia hatimaye zitafeli.
Dkt Fred Matiang'i, waziri wa zamani wa mambo ya usalama wa ndani Kenya//Maktaba

WAZIRI wa zamani wa elimu ya masuala ya usalama wa ndani, Dkt Fred Matiang’i ametua nchini usiku wa Alhamisi.

Matiang’i ambaye amekuwa akisemekana kulenga urais wa 2027 kwa tikiti ya chama cha Jubilee alilakiwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka eneo la Gusii lakini pia katibu mkuu wa chama hicho.

Katika picha ambazo zimechapishwa mitandaoni, Matiang’i alionekana mwingi wa furaha Pamoja na katibu wa Jubilee Jeremiah Kioni, seneta wa Kisii Richard Onyonka miongoni mwa wengine ambao wamekuwa wakimpigia debe.

Kwa muda mrefu sasa, Matiang’i ambaye ni mwandani wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta amekuwa akisemekana kulenga kutwaa uongozi wa ikulu katika uchaguzi wa 2027 japo mwenyewe hajawahi sikika akitamka kuhusu azma hiyo.

Ujio wake unatarajiwa kubadilisha kabisa mawimbi ya siasa za humu nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, ambapo Matiang’i huenda akaungana na wanasiasa wengine wengi kwa lengo la kumng’atua rais Ruto mamlakani kupitia kura za urais 2027.

"Mifumo yote iko tayari sasa!," Jubilee ilichapisha kwenye kurasa zake rasmi.

Kioni, haswa, amesisitiza mara kwa mara Matiangi kuongoza chama katika kinyang'anyiro kifuatacho cha uchaguzi.

Pia alionya dhidi ya majaribio ya kukwamisha azma ya Matiangi ya kisiasa, akisisitiza kuwa juhudi zozote za kumzuia hatimaye zitafeli.

Hata hivyo, wapinzani wa rais Ruto hawatakuwa na kibarua rahisi kumng’atua mamlakani wasipojipanga kwa njia sahihi.

Tayari rais Ruto ameweka wazi kwamba yuko tayari kumenyana na yeyote atayaeleng’a kumng’atua ofisini kupitia kwa kura, akionyesha matumaini kwamba wananchi watampa muhula wa pili kwa kuzingatia miradi ya maendeleo ambayo anapanga katika sehemu mbalimbali nchini.

Matiang’i sasa anatarajiwa kuungana na wapinzani wengine wa serikali akiwemo Kalonzo, Gachagua, Wamalwa, Karua, Omtatah na Kebaso kwa lengo la kutwaa ushindi 2027.

 

 

 

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved