Sherehe ya uzinduzi ilifanyika karibu na bwawa hilo katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz kusherehekea kukamilika rasmi kwa mradi huo.
Ujenzi wa mradi huu wa kuzalisha umeme wa megawati 5,150 ulianza mwaka 2011 katika Mto Blue Nile karibu na mpaka wa Sudan.
Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025, inaonyesha nyaya za kusafirisha umeme za Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz, Ethiopia. Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika. (Xinhua/Michael Tewelde)Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian
Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika.
Sherehe ya uzinduzi ilifanyika karibu na bwawa
hilo katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz kusherehekea
kukamilika rasmi kwa mradi huo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa
Ethiopia, viongozi wa Afrika na wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika na mashirika
mengine ya kimataifa, akiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali
Youssouf, Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh na
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Ujenzi wa mradi huu wa kuzalisha umeme wa
megawati 5,150 ulianza mwaka 2011 katika Mto Blue Nile karibu na mpaka wa
Sudan.
Akihutubia hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Abiy Ahmed alisisitiza uwezo wa bwawa hilo kuimarisha uchumi wa taifa kwa kutoa
nishati ya uhakika kwa viwanda, kuboresha maisha ya wananchi na kuendeleza
ushirikiano wa kikanda wa nishati.
“Hongera kwa Wethiopia wote, walio nyumbani na
walioko ughaibuni, pamoja na marafiki wetu duniani kote, kwa uzinduzi huu wa
kihistoria wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance,” alisema.
Mradi huo, wenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya
mita za ujazo bilioni 74 za maji, umekuwa chanzo cha mvutano mrefu kati ya nchi
tatu zinazotegemea Mto Nile: Ethiopia, Misri na Sudan.
Wakati Cairo na Khartoum
zikiogopa bwawa hilo litapunguza mgao wao wa maji, Addis Ababa imesisitiza
kwamba mradi huo hautadhuru nchi zilizoko chini ya mto.
“Ni waumini thabiti wa maendeleo ya pamoja,”
alisema Abiy, akithibitisha tena dhamira ya Ethiopia ya kufanikisha ukuaji bila
kudhoofisha maslahi ya majirani zake.
Mto
Blue Nile, unaojulikana nchini Ethiopia kama Mto Abay, unatokea katika Ziwa
Tana takribani kilomita 570 kaskazini mwa Addis Ababa na ni mojawapo ya mito
mikuu miwili inayounda Mto Nile.
Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025, inaonyesha Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz, Ethiopia. Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika. (Xinhua/Michael Tewelde)Rais wa Kenya William Ruto akizungumza katika hafla iliyofanyika karibu na Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz, Ethiopia, Septemba 9, 2025. Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika. (Xinhua/Michael Tewelde)
Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025, inaonyesha mto ulio chini ya Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz, Ethiopia. Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika. (Xinhua/Michael Tewelde)
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akizungumza katika hafla iliyofanyika karibu na Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) katika eneo la kaskazini magharibi la Benishangul-Gumuz, Ethiopia, Septemba 9, 2025. Ethiopia siku ya Jumanne ilizindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Afrika. (Xinhua/Michael Tewelde)