Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, Joseph Ogidi almaarufu Gidi Gidi yuko katika hali ya majonzi kufuatia kifo cha mtu wa karibu wa familia yake.
Gidi alifichua habari za kusikitisha kuhusu kifo cha binamu yake Ouma Odek siku ya Jumatano asubuhi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Katika taarifa yake, aliomboleza mwanamume huyo aliyemtaja kama kaka yake akisema kifo chake ni pigo kubwa sana.
“Tumempoteza kaka, hii imepiga sana. Pumzika kwa amani Ouma Odek,” Gidi aliandika chini ya picha yake, marehemu binamu yake na wanafamilia wengine.
"Wuod Kanyamwa nind gi kwe," aliongeza kwa lugha ya Kiluo.
Kumaanisha: "Mtoto wa Kanyamwa, lala salama.”
Mtangazaji mwenza wa Gidi, Jacob ‘Ghost’ Mulee ni miongoni mwa watu waliomfariji yeye na familia kufuatia habari hizo za kusikitisha.
“Poleni sana. Roho yake ipumzike kwa amani,” Ghost alimwandikia Gidi.
Tazama jumbe zingine kutoka kwa watumiaji wa mtandao;-
Harriet Achieng Nancy: Rambirambi zangu kwako na familia yako.
Kithe Senior: Mambo mazuri kweli hayakai muda mrefu, pumzika kwa amani kaka.
Ustadh Ali Mazrui: Pole sana kwa msiba Gidi.
Lum Amunga: Pole kaka yangu Joe Gidi kwa msiba. Yote ni sawa
Benard Were: Tulifanya mambo mengi wakati muda ulikuwa bado upande wetu.