logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wetang’ula amtambua Junet Mohamed kiongozi wa wengi bungeni

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa amekuwa akihudumu kama kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa.

image
na Davis Ojiambo

Hivi Punde11 February 2025 - 15:52

Muhtasari


  • Wetangula ambaye siku ya Jumanne alikuwa akisoma majina ya wabunge waliotuzwa wakati wa sherehe za Jamhuri mwaka jana alimtaja Junet kama kiongozi wa chama chenye wabunge wengi katika bunge la kitaifa.

Spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula amemtambua Junet Mohamed kama kiongozi wa wa wengi bungeni.

Wetangula ambaye siku ya Jumanne alikuwa akisoma majina ya wabunge waliotuzwa wakati wa sherehe za Jamhuri mwaka jana alimtaja Junet kama kiongozi wa chama chenye wabunge wengi katika bunge la kitaifa.

Hatua hii ya Wetangula inajiri siku chache baada ya mahakama kufutilia mbali uamuzi wa awali kuwa muungano Kenya Kwanza ndio uliokuwa upande wa wengi bungeni.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa amekuwa akihudumu kama kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa kufuatia uamuzi uliyokuwa umetolewa na spika Moses Wetangula.

Mahakama kuu manamo Februari, 7 2025 ilikosoa uamuzi wa Spika Wetang'ula kuwa muungano wa Kenya Kwanza ndio upande wa wengi katika Bunge hilo.

Jopo la majaji watatu lililojumuisha Majaji John Chigiti, Jairus Ngaah na Lawrence Mugambi liliamua kuwa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya ndio muungano wa wengi katika Bunge la Kitaifa.

Katika uamuzi wa kihistoria, mahakama ilisema Wetangula alikosea alipoupa muungano wa Kenya Kwanza wanachama 14 wa muungano wa Azimio ambao walikuwa wamejiuzulu kutoka kwa huo.

Wetangula alidai kuwa wanachama kadhaa wa Azimio waliiandikia afisi yake kusitisha uhusiano wao na chama cha Azimio la Umoja One Kenya.

Wabunge hao 14 walitoka katika vyama 4 chini ya Azimio, ambavyo ni United Democratic Movement (UDM), Movement for Democracy and Growth (MDG), Maendeleo Chap Chap (MCC) na Pamoja African Alliance (PAA).

Lakini jopo la majaji hao lilisema alipotia saini hati ya kiapo mahakamani kupinga kesi hiyo, hakutoa ushahidi wowote wa makubaliano yoyote ya baada ya uchaguzi yanayohusisha vyama vilivyotajwa na muungano wa KK.

Wetangula alidai kuwa vyama hivyo vilitia saini na kuweka kwa msajili wa vyama vya siasa mikataba hiyo.

Lakini majaji walikariri kwamba kwa kukosekana kwa uthibitisho wowote, uamuzi wa Wetang'ula hauwezi kuruhusiwa kusimama.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved