Mwanahabari Richard Quest wa CCN amuoa ndume mwenzake

Muhtasari

• Wawili hao walipeana posa mwezi Mei mwaka 2019, baada ya mpenzi wake kukubadi posa ya mwanahabari huyo.

• Tulisema  ‘I Do’ mwishoni mwa wiki. Siku bora zaidi katika maisha yetu.

• 2018, Quest alikataa kuomba msamaha kwa kukosoa hatua ya kuwabagua watu wenye uhusiano wa jinsia moja nchini Kenya.

Mwanahabari wa CNN Richard Quest hatimaye amefunga pingu za maisha na mpenziwe wa kiume Chris Pepesterny. 

Mwandishi huyo tajika wa habari ya biashara alizamia mitandao ya kijamii akielezea furaha yake kwa kusema "I DO" kwa barafu yake ya roho ambaye ni mwanamume mwenzake Chris na kuposti picha maridadi akiwa naye.

Quest aliandika kwa ujumbe wake; "Tulisema  ‘I Do’ mwishoni mwa wiki. Siku bora zaidi katika maisha yetu."

Wapenzi hao wawili walilazimika kuahirisha harusi yao mwezi Machi mwaka huu lakini wakaahidi kufunga ndoa kabla ya mwaka huu kuisha. 

"Leo Chris na mimi tulikuwa tuoane mjini London. Lakini ilibidi tuahirishe. Ni hatua ya kusikitisha lakini ilibidi. Tutaoana baadaye mwaka huu katika hafla kubwa...," alisema wakati wakiahirisha harusi yao. 

Wawili hao walipeana posa mwezi Mei mwaka 2019, baada ya mpenzi wake kukubadi posa ya mwanahabari huyo.

Mtangazaji huyo wa makala ya 'Quest Means Business' alizuru Kenya Oktoba 2018 ambapo alifunguka kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi.

Katika mahojiano kwenye radio Quest alisema kwamba hataomba msamaha kwa kukosoa hatua ya Kenya kuwabagua watu wenye uhusiano wa jinsia moja.