Chuo kikuu cha Afghanistan kitatenganishwa kwa jinsia na aina mpya ya mavazi ambayo yatatambulishwa, imesema Taliban.
Waziri wa elimu ya juu Abdul Baqi Haqqani ameeleza kuwa wanawake wataruhusiwa kusoma lakini hawatasoma pamoja na wanaume.
Pia alitangaza masomo ambayo yatakuwa yanafundishwa.
Wanawake na wasichana walipigwa marufuku kusoma shule na vyuo chini ya sheria ya Taliban kati ya mwaka 1996 na 2001.
Taliban imesema haitazuia wanawake kupata elimu au kuwa na ajira. Lakini tangu wamechukua taifa hilo Agosti 15, wamewataka wanawake wote isipokuwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya afya kutofanya kazi mpaka hali ya kiusalama itakapoimarika.
Tangazo la Jumapili kuhusu sera ya elimu ya juu limejiri siku moja baada ya Wataliban kupandisha bendera yao katika Ikulu ya rais, ikionesha ishara ya mwanzo wa utawala wao.
Walichukua udhibiti wa taifa hilo kutoka serikali iliyochaguliwa mwezi mmoja uliopita.
Sera hii inaashiria mabadiliko makubwa yanayotokana na kukubalika kwa kile kilichokuwa kinafanyika kabla ya Taliban kuchukua madaraka.
Wanafunzi wasichana walikuwa hawapewi kipingamizi cha mavazi na vyuo vikuu vilikuwa na wanafunzi mchanganyiko wanaume kwa wanawake.
Lakini bwana Haqqani hakuonesha kusikitishwa na maamuzi hayo. "Hatuna tatizo katika kusitisha mfumo wa elimu ya mchanganyiko ," alisema. "Watu wetu ni waislamu hivyo watakubali."
Baadhi walitoa mapendekezo yao kuwa sheria mpya zitawatenga wanawake katika kupata elimu kwa sababu vyuo havina rasilimali za kutosha kwa ajili ya kuwa na madarasa tofauti.
Hata hivyo bwana Haqqani alisisitiza kuwa kuna walimu wa kike wa kutosha na kama hawatatosha watatafuta mbadala.
"Inategemea na uwezo wa chuo ," alisema. "Tuaweza kutumia walimu wanaume kufundisha nyuma ya pazia au kutumia teknolojia."
Wasichana na wavulana pia watatengwa katika shule za msingi na sekondari, kitu ambacho kilikuwa kimezoeleka Afghanistan kote.
Wanawake watatakiwa kuvaa hijabs, hata hivyo bwana Haqqani hakufafanua kama itakuwa lazima kuwa hijabu za kufunika uso au la.
Waziri mpya aliyewekwa alisema masomo ambayo yatafundishwa chuo kikuu yatapitiwa upya.
"Aliwaambia waandishi kuwa Taliban inataka kutengeneza mtaala unaofaa na wa Kiislamu kulingana na Waislamu wetu ", maadili ya kitaifa na ya kihistoria na, kwa upande mwingine, kuweza kushindana na nchi zingine.
Tangazo hilo limekuja baada ya maandamano yaliyofanywa na wanawake kuunga mkono sera ya jinsia ya Taliban katika chuo kikuu cha Shaheed Rabbani huko Kabul .
Mamia ya wanawake , wengi wao wakiwa wamevalia hijabu nyeusi na kushika bendera ndogo ya Taliban, walisikiliza hotuba na kusifia mfumo mpya na kuwashutumu wale waliokuwa wanaandamana kutakahaki za wanawake kulindwa.
Tangu Taliban iondolewe madarakani mwaka 2001, kuna mabadiliko makubwa yamepatikana katika kuboresha elimu ya Afghanistan na viwango vya kusoma - haswa kwa wasichana na wanawake.
Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa mataifa (UN) ilisema idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka katika shule za msingi kutoka sifuri mpaka milioni 2.5 katika miaka 17 baada ya ya utawala wa Taliban .
Ripoti ilisema pia kiwango cha elimu kimeongezeka mara mbili katika muongo kwa 30%.
Serikali mpya ya Taliban imebadilisha waziri wa masuala ya wanawake kuwa wizara ya makamu na uadilifu.
Hofu kubwa ni kuwa idara iliyokuwa inashughulikia kupeleka polisi kuhamasisha sheria ya kiislamu kufuatwa wakati wa utawala wa awali wa Taliban ndio inawajibika sasa.
Ilifahamika kwa kuwapiga wanawake kwa kutovaa kiheshima na kuwa nje bila ya mwanaume anayemuangalia.
Wanawake wengi maarufu wenye elimu walikimbia Afghanistan wakihofia kwa utawala wa awali utarudi. Mwimbaji mkubwa wa miondoko ya pop Aryana Sayeed aliondoka taifa hilo na kwenda Marekani kwa kutumia ndege ya mizigo na muongozaji wa filamu Sahraa Karimi alikimbilia Ukraine