
Kiongozi wa Katoliki duniani Papa mtakatifu Francis ataendelea kubakia hospitalini wakati akiendelea kupokea matibabu hili ni kulingana na habari kutoka Vatican.
Mji wa Vatican ni makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Roma, serikali ya dini na serikali ya nchi. Mkuu wa nchi au mtawala ni Papa ambaye ni, Askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki la Kirumi. Papa Francis, kardinali wa zamani wa Jorge Mario Bergoglio, alichaguliwa tarehe 13 Machi 2013.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 88 alilazwa katika hospitali ya Gemelli mjini Rome siku ya Ijumaa ili kufanyiwa matibabu na vipimo vya ugonjwa wa bronchitis.
Siku ya Jumatatu, Vatican ilisema kuwa Papa ana "maambukizi ya njia yake ya kupumua" ambayo yamehitaji mabadiliko katika matibabu yake.
Taarifa ya baadaye iliongeza kuwa Papa alikuwa "anaendelea na matibabu yaliyoagizwa" katika hali thabiti na hakuwa na homa. Pia alifanya kazi na kusoma akiwa hospitalini siku ya jana Jumatatu.
"Kabla ya kuingia kwake wiki iliyopita, Papa alikuwa na dalili za ugonjwa wa bronchitis kwa siku kadhaa na alikuwa akiwapa maafisa kusoma hotuba zilizotayarishwa katika hafla.
"Anataka kutoa pole zake kwa wale waliolazwa hospitalini kwa wakati huu, kwa upendo waliouonyesha kupitia michoro na ujumbe wa matakwa mema; Anaomba kwa ajili yao nao waomba kwa ajili yake." ujumbe uliongeza,
Msemaji wa Vatican Matteo Bruni pia aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba Papa yuko katika hali nzuri.
Taarifa fupi juu ya hali yake ilisema: "Vipimo vyote vilivyofanywa hadi sasa vimetoa ishara ambayo itahitaji kulazwa hospitalini na ujumbe wa kila wiki wa Papa, ambao kwa kawaida hufanyika kila Jumatano, umefutiliwa mbali wiki hii.
Mwishoni mwa wiki, Vatican ilisema Papa alikuwa imara na kwamba aliambiwa " apate kupumzika vizuri" ili kusaidia kupona kwake.
Papa amelazwa hospitalini mara kadhaa katika kipindi cha miaka 12 kama kiongozi wa Kanisa Katoliki pia amekumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya katika maisha yake yote, ikiwa ni pamoja na kuondolewa sehemu ya mapafu yake akiwa na umri wa miaka 21.
Mnamo Machi 2023, alilazwa siku tatu hospitalini kutokana na bronchitis na mnamo Juni mwaka huo alifanyiwa upasuaji wa saa tatu ili kurekebisha hernia ya tumbo [abdominal hernia].
Mwezi Desemba mwaka jana alionekana na michubuko mikubwa kwenye kidevu chake wakati alipoongoza sherehe katika kanisa la St Peter's Basilica ya kuweka makadinali wapya 21 wa Kanisa Katoliki, ambayo Vatican ilisema ni matokeo ya kuanguka kidogo.
Ugonjwa mwingine pia ulimlazimisha kufuta safari yake ya kwenda Falme za Kiarabu kwa mkutano wa hali ya hewa wa COP28 mnamo 2023. Hivi karibuni, mwezi Januari alianguka na kuumiza mkono wake wa kulia.