
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro na rais wa Marekani Donald Trump
Viongozi wa Ulaya walikumbwa na Taharuki kubwa na sera za uongozi wa Rais Trump wa Marekani baada ya wao kutoalikwa katika mkutano wa majadiliano na Urusi kuhusu mustakabali wa Ukraine.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kuwa anapanga kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin ili wawe na majadiliano kuhusu taifa la Ukraine.
Jumatatu Waziri mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer alisema Uingereza iko tayari na ina hamu kubwa ya kutaka kutuma jeshi la ardhini,msemaji wa masuala ya kigeni wa nchi ya Ujerumani alisema kuwa taifa hilo liko tayari kutuma vikosi vya usalama ndani ya mfumo wa Kimataifa.
Mataifa hayo yalielezea kuwa utawala wa Trump haukukuwa na uhakika asilimia 100 kuhusu kile kinachopaswa kufanywa kuhusu taifa la Ukreini.
Hii ni fursa finyu sana kwa Ulaya ikijaribu kumshawishi Trump ambaye ni mshirika mkubwa katika suala hili la Ukreini na Urusi.Ambapo Ulaya imekuwa ikisisitiza kuwa hakuna maamuzi yatakayotolewa bila taifa la Ukreini kushirikishwa moja kwa moja.
Mataifa hayo ya Ulaya yalishangwa na usemi wa Rais Trump kuwa asingeshirikisha baadhi ya mataifa ya wanachama wa usalama.Kwa muda sasa Ulaya imekuwa ikitegemea kivuli cha usalama kilichotolewa na Marejkani tangu vita vya pili vya dunia.
Kulingana na Vigezo vya majadiliano ya Urusi na Marekani kuhusu Ukreini na jinsi ambavyo rais Putin amekuwa akijihisi kuwa na nguvu kutokana na hayo kuna hofu ya Ulaya kuwa hilo linaweza kubadilisha ufanisi wa usalama wa bara lao.
Kwa muda mrefu Putin kihistoria huchukia upanuzi wa Nato kuelekea nchi za Mashariki, kwa hivyo nchi ndogo Jirani na urusi kama Baltiki na Polandi zinahisi kuwa hatarini.
Nchi za ulaya zikijumuisha Ufaransa,Ujerumani na Uingereza zinaazimia kuwa na mkutano mjini parisi Ufaransa ili kujadili hatima ya Ukreini ila hofu yao ni kuwa je, Marekani itawaunga mkono katika suala la kuleta amani na ujulivu katika nchi hiyo?.
Hii inatokana na wito wa Trump kuitisha mkutano na rais wa Urusi pasi kuyajumuisha mataifa mengine ya wanachama jambo ambalo linaibua maswali mengi kuhusu mkutano huo wa Marekani na Urusi.