
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 21 amefunguliwa mashtaka baada ya kuchomwa moto nyumba ya mchumba wa mpenzi wake wa zamani.
Tukio hilo lilifanyika katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani
ambapo inaarifiwa kwamba Harrison Jones, 21, alisafiri umbali wa kilomita 1126
kutoka jimbo la Michigan kutekeleza kisasi hicho.
Katika mkasa huo wa moto, watu wazima 6 walijeruhiwa huku
mbwa 2 wakiteketea hadi kufa.
Watu wazima sita katika nyumba hiyo walikuwa tayari
wameokolewa, wengine wakilazimika kuruka kutoka orofa ya pili ya nyumba ili kujiokoa,
kulingana na polisi.
Mshukiwa huyo anadaiwa kuendesha gari kwa takriban saa 12
kutekeleza uhalifu huo ambao karibu ulichukua maisha ya watu sita.
Mamlaka haijatoa utambulisho wa waathiriwa sita na
haijulikani ni kiasi gani majeraha yao ni makubwa.
Walisafirishwa hadi hospitali ya eneo hilo wakati vyombo vya
sheria vilipofika. Nyumba iliyoharibiwa ilikuwa ya familia moja ya ghorofa
mbili.
Watekelezaji wa sheria walishuku kuwa moto huo haukuwa wa
bahati mbaya na walianza kupitia kanda za usalama ili kumpata anayedaiwa kuwa
mchomaji.
Video ya uchunguzi kutoka kwa nyumba iliyo karibu ilinasa
sedan nyeusi ikipita nyumbani kwenye Merganser Way. Picha hiyo ilifichua mtu
akitoka kwenye gari na kuelekea nyumbani kabla ya kuungua saa 5:01 asubuhi,
vyombo vya habari vilisema.
Baada ya dakika kumi na tano, mtu huyo alionekana akikimbia
kurudi kwenye gari huku moshi ukifuka angani nyuma yake.
Mlipuko mkubwa uliweza kusikika wakati mshukiwa aliyechoma
moto akikimbia eneo la uhalifu.
Polisi walikamata gari hilo aina ya Volkswagen Passat na
kupata vifaa vya kuokota kufuli, simu ya rununu na kompyuta.
Mshukiwa pia aliripotiwa kuungua mkono wakati polisi
walipomkabili, kulingana na polisi.
Harrison alikamatwa na kushtakiwa kwa Jaribio la Mauaji ya
Jinai, Uchomaji moto, na Janga la Kuhatarisha. Maafisa wa kaunti ya Kent
wanamshikilia mshukiwa huyo huku akisubiri kurejeshwa Pennsylvania.