
RAIS wa Rwanda Paul Kagame ameyaambia mataifa yanayopendekeza Rwanda kuwekewa vikwazo ‘kuenda kuzimu’, wiki kadhaa baada ya baadhi kutaka mataifa ya Magharibi kuwekea Rwanda vikwazo vikali kutokana na kudaiwa kuhusika katika mzozo wa vita mashariki mwa DRC.
Akihutubia taifa
wakati wa kuadhimisha miaka 31 tangu mauaji ya kimbari vya 1994 nchini Rwanda,
rais Kagame alisema kwamba wananchi wa Rwanda wataishi kwa njia ambayo
wanaitaka wenyewe bila kupangiwa na mtu yeyote kutoka nje.
Rais Paul Kagame
na mke wa rais Jeannette Kagame, akijumuika na mkuu wa mabalozi katika mji mkuu
Kigali na wawakilishi wa manusura wa mauaji ya halaiki, waliweka mashada ya
maua kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Kigali, ambapo zaidi ya wahanga
250,000 wamezikwa.
Kisha wakawasha
"Mwali wa Kumbukumbu," ishara ya umoja wa kitaifa na ujasiri, ambayo
itawaka kwa siku 100 zijazo - urefu wa mauaji ya kimbari.
Kagame alisema
mauaji ya kimbari hayatatokea tena nchini Rwanda - sio kwa sababu wahalifu
hawatajaribu, lakini kwa sababu "Wanyarwanda wamechagua kusimama pamoja na
ili yasitokee tena."
Katika hotuba
yake, Kagame alihusisha zamani za Rwanda na changamoto zake za sasa, akisema
"ni ndugu" ambazo lazima zishughulikiwe pamoja.
Alikuwa
akizungumzia mvutano wa kidiplomasia na nchi zinazoituhumu Rwanda kuhusika
katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kagame alikosoa
shinikizo la kimataifa kuhusu suala hilo, akisema: "Nenda kuzimu."
"Hawa
watu wa UN, katika miji mikuu hii ya Magharibi, wakisema nchi hii ndogo, Rwanda
hii, wakati mnakusanyika pamoja dhidi ya Rwanda ... nafikiria tu ulimwengu
umeharibika. Lakini katikati ya yote tunayopaswa kuishi, na nitamwambia mtu
yeyote usoni mwake aende kuzimu. Mtu yeyote akija karibu na kufikiri anaweza,
unajua, wanakuja na kusema 'hey we're going to sanction. Nenda kuzimu,” alisema.
Umoja wa Ulaya
umewawekea vikwazo maafisa watatu wakuu wa jeshi la Rwanda na mkuu wa wakala wa
uchimbaji madini wa serikali ya Rwanda juu ya kundi la waasi la M23 kisa mzozo
wa Kongo.
Ujerumani,
Marekani na Uingereza pia zilitangaza kuiwekea Rwanda vikwazo kwa madai ya
kuhusika kwake mashariki mwa Kongo.
Rwanda mwezi
uliopita ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji baada ya Kagame
kuishutumu Brussels kwa kushawishi kuiwekea vikwazo vya kimataifa Kigali.