
Mpango wa Maendeleo ya Kimataifa unaangazia mahitaji ya pamoja ya maendeleo ya binadamu, na unakabiliana moja kwa moja na changamoto halisi za maendeleo.
Mpango wa Usalama wa Kimataifa umejikita katika kuondoa mizizi ya migogoro ya kimataifa na kuboresha utawala wa usalama wa dunia.
pango wa Ustaarabu wa Kimataifa unatoa mfumo unaowezesha nchi kufuata njia za uboreshaji wa kisasa zinazojikita katika tamaduni zao wenyewe huku zikiwa wazi kwa hekima ya pamoja ya binadamu.
Mpango wa Utawala wa Kimataifa unasisitiza usawa wa mamlaka ya nchi, ukilenga moja kwa moja mapungufu ya mfumo ambamo “nchi chache ndizo hutoa maamuzi.”

Kabla ya hapo, Beijing ilikuwa tayari imependekeza mfululizo wa mipango mikubwa ya dunia: Mpango wa Maendeleo ya Kimataifa (GDI) mwaka 2021, Mpango wa Usalama wa Kimataifa (GSI) mwaka 2022, na Mpango wa Ustaarabu wa Kimataifa (GCI) mwaka 2023. Kwa pamoja na GGI, mipango hii inaunda mfumo kamili wa kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu.
Kila mpango unashughulikia nguzo muhimu ya ushirikiano wa kimataifa: GDI inalenga kuweka msingi wa kimaada, GSI inalenga kulinda uthabiti, GCI inalenga kukuza uelewano wa pamoja, huku GGI ikilenga kutoa mfumo wa kitaasisi. Kama alivyonukuliwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mipango hiyo minne ya dunia iliyopendekezwa na China “inaendana kikamilifu na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.” Nchi nyingi pia zinaiona kama suluhu za vitendo na zenye kujenga katika kukabiliana na changamoto za sasa za dunia.

Maendeleo ya dunia bado ni dhaifu, yakikumbwa na kuongezeka kwa pengo kati ya Kaskazini na Kusini, sambamba na misukosuko ya pamoja ya nishati na chakula. Zaidi ya watu bilioni 1 duniani wanaishi katika umaskini wa kupindukia. Usalama nao unazorota, huku migogoro ya silaha ikifikia viwango vya juu tangu vita vikuu, ongezeko la watu waliokimbia makazi yao, na matumizi yanayoongezeka ya vikwazo na vitisho kutoka kwa baadhi ya nchi.
Wakati huo huo, mjadala wa “mgongano wa ustaarabu” unaonekana kutawala badala ya maingiliano kati ya ustaarabu, huku utawala wa dunia ukidhoofishwa na kujitoa kwenye mikataba ya kimataifa, sera za kujitenga kiuchumi, na ujenzi wa vikwazo vinavyodhoofisha haki na usawa, hasa kwa nchi za Kusini mwa Dunia.
Uhalisia huu mgumu unaonesha umuhimu na uharaka wa mipango minne ya dunia, na kuangazia haja ya kujenga makubaliano ya kimataifa na kuimarisha mshikamano.
WITO WA MAENDELEO YA PAMOJA
Kama alivyoeleza Xi, maendeleo ndiyo ufunguo mkuu wa kutatua matatizo yote. Mpango wa Maendeleo ya Kimataifa unalenga mahitaji ya pamoja ya maendeleo ya binadamu, unaendana kwa karibu na Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya 2030, na unakabiliana moja kwa moja na changamoto halisi za maendeleo ya dunia. Mpango huu unachangia hekima na suluhu za China katika kuendeleza kwa pamoja maendeleo ya dunia kuelekea hatua mpya ya ukuaji wenye uwiano, uratibu na ujumuishaji.

Kwa kiwango cha dunia, maendeleo yanarudi nyuma katika maeneo muhimu. Umaskini wa kupindukia umeongezeka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo miwili, huku nusu maskini zaidi ya binadamu wakimiliki asilimia 2 tu ya utajiri wa dunia. Takriban watu bilioni 2.6 bado hawana huduma ya intaneti, na pengo la ufadhili kwa nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi linaendelea kupanuka.
Zaidi ya hayo, vita na migogoro vimewasukuma watu milioni 140 katika uhaba mkubwa wa chakula, huku vikwazo vya upande mmoja vikiathiri pakubwa maisha ya mabilioni ya watu.
Takwimu hizi zinabainisha dosari za kimsingi katika mfumo wa maendeleo ya dunia. Baadhi ya nchi zilizoendelea zimeweka maslahi ya kijiografia mbele ya ushirikiano, zikinyonya rasilimali za maendeleo kupitia vikwazo, kujitenga kiuchumi na kupunguza misaada. Kwa kufanya hivyo, zimeisaliti kauli ya pamoja ya kimataifa kwamba haki ya maendeleo ni haki ya msingi ya binadamu.
Muundo usio na uwiano wa utawala wa dunia umeacha nchi zinazoendelea zikiwa na nafasi ndogo katika kutunga sheria za kimataifa, huku vizuizi vya kiteknolojia na biashara vikiendelea kupanua pengo la maendeleo.

Changamoto hizi si tu zimeongeza hatari ya kushindwa kwa Ajenda ya 2030, bali pia zimeonesha haja ya dharura ya hatua mahsusi kukabiliana na matatizo ya maendeleo ya dunia.
Mpango wa GDI, uliopendekezwa katika wakati huu muhimu, umepata mvuto mkubwa duniani kwa kuvunja mtazamo wa kizamani ambapo mataifa makubwa hutawala na mataifa madogo hulazimika kuyategemea. Pia unakuza hatua za pamoja kwa misingi ya usawa na mtazamo wa kimfumo, kuhakikisha kila mshiriki ananufaika na maendeleo.

Kituo cha Maonesho ya Teknolojia ya Kilimo cha China-Afrika kinatumia mtindo wa “kufundisha mtu kuvua samaki,” na kimeongeza wastani wa mavuno ya mazao kwa asilimia 30–60, kikinufaisha zaidi ya wakulima milioni moja.
Reli ya China–Laos imeigeuza Laos kutoka nchi isiyo na bandari kuwa kitovu cha usafirishaji, ikipunguza gharama za usafirishaji kwa zaidi ya asilimia 30 na kuunda zaidi ya ajira 100,000. Vilevile, vituo vya pamoja vya ubunifu wa teknolojia kati ya China na Brazil vimeimarisha ulinzi wa mazingira na kupanua upatikanaji wa nishati safi kwa jamii za mbali.
Zaidi ya kuipa Ajenda ya 2030 msukumo mpya, GDI inabadilisha na kuunda upya dhana za maendeleo ya dunia, ikijitenga na utegemezi wa mifumo ya jadi ya Magharibi na kuweka mbele maslahi ya pamoja ya binadamu.
NJIA MPYA YA AMANI NA USALAMA WA KUDUMU
Dunia ya leo inapitia misukosuko na mageuzi makubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi. Upungufu wa amani na usalama unaongezeka, na utawala wa usalama wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa.

Historia inaonesha kuwa kutafuta usalama wa hali ya juu kwa nguvu na kuunda mifumo ya kipekee ya usalama ni sawa na “sheria ya msituni,” ambayo mara kwa mara imeleta maafa makubwa.

China imekuwa mstari wa mbele katika upatanishi wa migogoro na ni mchangiaji mkubwa zaidi wa vikosi vya kulinda amani miongoni mwa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
HESHIMA KWA TOFAUTI ZA USTAARABU

JARIBIO JIPYA LA UTAWALA BORA WA DUNIA
Mpango wa Utawala wa Kimataifa unalenga kurekebisha mapungufu ya mfumo wa sasa wa utawala wa dunia kwa kusisitiza usawa wa nchi, kuheshimu sheria za kimataifa, kuimarisha mfumo wa pande nyingi na kuweka ustawi wa watu mbele.


