logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kesi ya pili yawasilishwa dhidi ya ada mpya za stakabadhi muhimu za serikali

Bikeri anasema Kindiki hakushirikisha umma kabla ya ada mpya kutangazwa.

image
na Davis Ojiambo

Habari14 November 2023 - 14:46

Muhtasari


  • • Jaji Lawrence Mugambi aliagiza mlalamishi kuwasilisha ombi lake kwa Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki na Mwanasheria Mkuu Justin Muturi.
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi

Ombi la pili limewasilishwa katika mahakama kuu ya Milimani likitaka kubatilisha notisi ya gazeti la serikali iliyochapishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ikiongeza ya ada na tozo za hati za kusafiria, vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa, ndoa na vifo. 

Mlalamishi Fredrick Bikeri anasema uchapishaji wa notisi ya gazeti la serikali la tarehe 6 Novemba 2023 unakiuka vifungu kadhaa vya katiba. 

Mlalamishi kupitia mawakili wake Shanice Maingi na Danstan Omari alisema kwamba atadhihirishia mahakamani kwamba waziri Kithure Kindiki alifanya kinyume cha sheria kwa kuchapisha notisi ya gazeti la serikali. 

Walisema hakushirikisha umma kama inavyotakiwa kisheria kabla ya tozo na ada mpya kutangazwa. Walisema nyongeza ya ada kutoka Shilingi 100 hadi Shilingi 1000 ni ya kiwango cha juu na Wakenya wengi hawatamudu hasa vijana wanaohitimu kidato cha nne na ambao wanahitaji vitambulisho kutafuta Kazi na masomo ya juu. 

Jaji Lawrence Mugambi aliagiza mlalamishi kuwasilisha ombi lake kwa Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki na Mwanasheria Mkuu Justin Muturi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved