Jamaa mmoja apigwa risasai na polisi akijaribu kumkata mamake

Polisi walisema waliingilia kati ili kumtuliza mtuhumiwa lakini badala yake alimgeukia OCS wapolisi.

Muhtasari

• Polisi walisema waliingilia kati ili kumtuliza mtuhumiwa lakini badala yake alimgeukia kamanda huyo kwa lengo la kumkata kichwani na jembe hilo.

Pingu
Image: polisi wawili washikwa kwa madai ya hongo

Mwanamume mwenye umri wa miaka 22 alipigwa risasi siku ya Jumanne na kuuawa na polisi baada ya kumvamia afisa mkuu wa polisi aliyejaribu kumzuia kumkata mamake mwenye umri wa miaka 68 nyumbani kwao eneo la Chekata, Kakamega.

Polisi walisema kwamba kakake mkubwa aliripoti katika kituo cha polisi cha Navakholo kwamba Ian Wanjala ambaye sasa ni marehemu alikuwa amejihami kwa panga, kisu na jembe na alikuwa akitishia kumuua mama yao.

Hilo lilimfanya afisa anayesimamia kituo hicho kuongoza kikosi cha maafisa hadi eneo la tukio.

Kulingana na polisi, walipofika, walimkuta mshukiwa akiwa na silaha akimfukuza mama huyo.

Polisi walisema waliingilia kati ili kumtuliza mtuhumiwa lakini badala yake alimgeukia kamanda huyo kwa lengo la kumkata kichwani na jembe hilo.

Kulingana na polisi, afisa huyo alikwepa na kuzuia kwa kutumia mkono wake wa kulia na kuvunjwa vidole viwili. Pia aliteleza na kuanguka huku akijaribu kukimbia hatari ya mashambulizi.

Hapo ndipo alipofikia bastola yake na kufyatua risasi huku mshukiwa akidaiwa kumfuata, polisi walisema. Afisa huyo alifyatua risasi hewani kumuonya mshukiwa, polisi walisema.

Mshukiwa, kwa mujibu wa polisi aliendelea kumfuata afisa huyo na katika harakati hizo, alimpiga risasi kifuani.

Mshukiwa na OCS walikimbizwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Navakholo ambapo mshukiwa alitangazwa kufariki alipofika.

OCS huyo alipewa matibabu ya huduma ya kwanza na kupelekwa katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Kaunti ya Kakamega huku mwili wa marehemu ukihamishiwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kakamega kusubiri uchunguzi wa maiti, polisi walisema.

Kikosi cha maafisa wa polisi kutoka Kakamega kinachunguza tukio hilo, polisi walisema.