logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya kuelekea jela wakati mkurugenzi wa mashtaka ya umma akiangazia genge lake lake

Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi ulio na uzito ulliomhushisha Akinyi na ulanguzi wa madawa za kulevya

image
na OTIENO TONNY

Mahakama29 November 2024 - 11:48

Muhtasari


  • Wachunguzi walifichua kwamba mshukiwa  aliendesha biashara hiyo haramu ambao ilikuwa imeajiri vijana wadogo wa  kiume na wa kike.
  • Akinyi alipata umaarufu wakati akijihusisha na ulanguzi wa heroine akiwa na mumewe wa wakati huo aliyekuwa raia wa Nigeria Anthony Chinedu.


Huku mfanyabiashara mwenye utata Joyce Akinyi akipatikana na hatia katika kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya, sasa joto  limeibuka kwa washirika wenzake  wenye nguvu ambao walijaribu kumkinga dhidi ya kukumbana na mkono wa kisheria.

Kwa miaka mitano iliyopita sasa imeibuka kuwa  watu ambao hawakutajwa majina lakini wanaaminiwa ni wenye  nguvu walijaribu kushawishi mchakato huo kuchukua mkondo tofauti.  Wakati fulani, walijaribu kwa makusudi kuwazuia waendesha mashtaka kuendelea na uchunguzi zaidi.

Timu ya upande wa mashtaka, ikiongozwa na Norah Achieng, Annette Wangia na Faith Mwila, iliwasilisha ushahidi ulio na uzito unaomhusisha Akinyi na operesheni ya kisasa ya kimataifa ya dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Renson Ingonga, alisema  kwamba kulikuwa na majaribio kadhaa ya kukwamiza na  kushawishi mchakato huo mzima.

Licha ya majaribio kadhaa kutoka kwa wandani wa mshukiwa kujaribu kuhitilafiana na  mchakato wa kumshtaki, bado idara ya mashtata ya umma ilisimama kidete kuendeleza mchakato huo.

 "Kulikuwa na majaribio mengi na watu wenye nguvu wanaotaka kushawishi waendesha mashtaka kwa njia moja au nyingine, lakini tulisimama imara kwa sababu tunataka kesi hii iwe onyo kwa walanguzi wowote huko nje kwamba tunawafuata na tutawapata,"  Alisema  Ingonga.

Ilibainika kuwa kulikuwa na majaribio kadhaa ya kushawishi mchakato huo na watu wenye umaarufu na nguvu nyingi zaidi

"Watu waliojaribu kuingilia kati wana nguvu na wana uhusiano mzuri. Ilijulikana kwa umma kuwa mshukiwa  amekuwa katika uhalifu huu kwa muda na amekuwa akidanganya sheria wakati huu wote kwa sababu ya watu wenye nguvu na ushawishi kumlinda. Mchezo walidhani wangecheza na sisi pia." Aliendelea kusema Renson Ingonga.

Kwa kuwa mshukiwa na wenzake wengine wanapitia mashtaka, mkrugenzi huyo wa mashtaka ya umma alisema kuwa atafanya kazi pamoja na maafisa wa polisi ili kuwafichua wahalifu wote ambao bado wanajificha.

Aliongeza kusema  kuwa watafanya juhudi kwa kushirikiana na maafisa wa polisi ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

"Lakini tutashirikiana na polisi na washirika wetu kuwafikia na kuwaweka wazi kwa ajili ya haki. Katika mahakama, tunataka hukumu ya kuumwa ambayo itatumikia onyo kwa watu hawa wenye kivuli,"  Ingonga aliongeza.kusema

Akinyi alipata umaarufu wakati akijihusisha na ulanguzi wa heroine akiwa na mumewe wa wakati huo aliyekuwa raia wa Nigeria Anthony Chinedu, ambaye alifukuzwa nchini humo mwaka 2014.

Uchunguzi ulifichua kwamba mshukiwa  aliendesha biashara hiyo haramu ambayo ilikuwa imeajiri vijana wadogo wa  kiume na wa kike ikibainika kuwa neno la mdomo lilitumika  kwa mawasiliano na  kutoa maagizo pekee.

Masoko yake ya usafirishaji yalikuwa hasa yale ya  nchi za Asia, ambapo baadhi ya watu katika kundi lake hawakuwa na bahati nzuri na kusababisha kukamatwa kwa wengine wao ambao bado wanahudumia kifungo wa miaka mingi .




RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved