
MSHAURI wa masuala ya uwekezaji mjamzito ameshinda zaidi ya £93,000 [Ksh 15,228,089] kama fidia baada ya bosi wake kumfukuza kazi na kisha kumtumia ujumbe wenye emoji ya "mikono ya jazz".
Kwa mujibu wa jarida la Telegraph, Ammar Kabir alimfukuza
kazi Paula Miluska kwa kumtumia ujumbe "usioeleweka kwa makusudi"
wakati akiwa mgonjwa, akielezea jinsi biashara "ilivyokuwa
inataabika" na kwamba ilihitaji kupata mtu ambaye anaweza "kuwa
ofisini", mahakama ilisikika.
Kufutwa kazi kwake kulikuja baada ya mama huyo mjamzito
kuomba kufanya kazi kutoka nyumbani kwa sababu alihisi “kichefuchefu" kwa
sababu ya ugonjwa wake wa kutapika kila asubuhi.
Alipokuwa akiwasilisha habari za kuachishwa kazi kwake, Bw
Kabir alimtumia ujumbe ulioishia na "Natumai kukuona hivi karibuni,
tumepata mengi ya kufanya nje ya kazi" ikifuatiwa na "tabasamu la
mikono ya jazz".
Emoji hiyo ilionyesha uso wenye tabasamu huku viganja viwili
vya mikono vikitazama nje na inasemekana kuonyesha hisia za msisimko na shauku.
Bi Miluska alituzwa fidia baada ya hakimu kuhitimisha kuwa
alifukuzwa kazi isivyo haki kutokana na ugonjwa wake wa ujauzito.
Mahakama ya uajiri ilisikia kwamba Bi Miluska alianza
kufanya kazi katika kampuni ya Roman Property Group Limited, iliyoko
Birmingham, mnamo Machi 2022.
Mnamo Oktoba mwaka huo, mshauri wa uwekezaji aligundua
kwamba alikuwa akitarajia mtoto na mwezi uliofuata, "alianza kuona madhara
ya ujauzito wake kwa namna ya ugonjwa wa asubuhi".
Jopo hilo lilisikia ujumbe ambao Bi Miluska alituma kwa
meneja wake Bw Kabir alipohitaji kuondoka kazini mapema kwa sababu ya
"kichefuchefu kilichoongezeka" aliokuwa nao wakati wa ujauzito.
Siku iliyofuata, alimtumia ujumbe uliosema: "Mkunga
alikuwa akisema kwamba kwa sasa ikiwa naweza kufanya kazi nyumbani itakuwa bora
kwani wiki mbili zijazo kawaida huwa kilele cha kichefuchefu cha ujauzito kutokana
na homoni.
Hakimu wa masuala ya uajiri alisema hakukuwa na "SMS
nyingine" kati ya wawili hao hadi Novemba 26, Bw Kabir alipomuuliza Bi Miluska
jinsi anavyohisi.