logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mfahamu muhubiri TB Joshua(<em>marehemu</em>)

Kulingana na Mtandao wa kanisa lake la SCOAN , Joshua alikuwa ndani ya tumbo la mamake kwa miezi 15 kabla ya kuzaliwa kwake

image
na Radio Jambo

Habari07 June 2021 - 04:36

Muhtasari


•Baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa kutokana na idadi ya miujiza yake anayofanya katika mikutano yake

•Kulingana na jarida la Forbes 2011 , Temitope Joshua ni muhubiri wa tatu tajiri nchini Nigeria akiwa na thamani ya $15m.

TB Joshua

Kifo cha mhubiri mashuhuri wa kimataifa Temitope Balogun Joshua maarufu kama T.B Joshua siku ya Jumapili kilishangaza wengi dunia nzima.

Kanisa lake la Sinagogi la mataifa yote SCOAN lililoanzishwa na muhubiri huyo lilithibitisha habari za kuhuzunisha za kifo chake Jumapili alfajiri likisema:.

Muhubiri TB Joshua anawacha sifa za huduma na kujitolea kwa ufalme wa Mungu ambao utaendelea kuwepo kwa vizazi vijavyo.

Muhubiri TB Joshua ni raia wa Nigeria kiongozi na mwanzilishi wa kanisa la SCOAN ambalo limekuwa likirusha matangazo yake mubashara katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos kusini mwa Nigeria.

Alizaliwa kama Temitope Balogun Joshua mnamo tarehe 12 mwezi Juni katika jimbo la Ondo nchini Nigeria.

Historia ya TB Joshua

Kulingana na Mtandao wa kanisa lake la SCOAN , Joshua alikuwa ndani ya tumbo la mamake kwa miezi 15 kabla ya kuzaliwa kwake.

Joshua alisomea katika shule ya msingi ya St. Stephen Anglican {Ikare-Akoko, Nigeria 1971-1977} lakini aliwacha shule alipojiunga na shule ya upili baada ya mwaka mmoja na kufanya kazi katika shamba moja la kuku

.Akiwa shuleni alijulikana kama muhubiri mdogo kutokana na alivyokuwa akiipenda Biblia na uwezo wa kutabiri matukio yaliofanyika katika jamii yake , kulingana na mtandao wa SCOAN.

Alianzisha kanisa la SCOAN mwaka 1987 akiwa na waumini wachache kabla ya kanisa hilo kupanuka hadi kimataifa.Mwaka 2009 TB Joshua alianzisha klabu ya kandanda kwa jina My people FC katika juhudi za kuwasaidia vijana.

Wanachama wawili wa timu hiyo Sani Emmanuel na Ogenyi Onazi walichezea Nigeria Golden mwaka 2009, katika kombe la dunia la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17.Tayari wachezaji watatu wamepata ufadhili Ulaya kuwa wachezaji wa kulipwa nchini Sweden.

Kulingana na jarida la Forbes 2011 , Temitope Joshua ni muhubiri wa tatu tajiri nchini Nigeria akiwa na thamani ya $15m.

Utata wa TB Joshua

Baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa kutokana na idadi ya miujiza yake anayofanya katika mikutano yake.

Baraza la makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria PFN , chini ya mwavuli wa makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria hayakubaliani na kanisa la muhubiri huyo wakimtaja TB Joshua kuwa kibaraka.

Christ Okote muhubiri wa kanisa maarufu nchini Nigeria alimshutumu Joshua kwa kuwa 'mganga'Wakosoaji wake wa Kikristo wanasema kwamba mbinu zinazotumiwa na Joshua haziendani na zile za biblia.

(Uhariri na Samuel Maina)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved