Lakini kuna zaidi ya viwango vya chini vya riba! Katika makala hii, tunafunua siri za kuwa mmiliki wa nyumba.
1. Fanya kazi na taasisi ya fedha inayoaminika.
Anza safari yako ya umiliki wa nyumba kwa hatua muhimu kwa kuchagua taasisi ya fedha yenye sifa dhabiti. Kwa ushirikiano na benki na mashirika ya mikopo KMRC inatoa tarakimu moja, viwango vya riba vilivyowekwa vinavyodumu kwa muda mrefu wa ulipaji. Viwango vya chini ya asilimia 10 vinafanya wakati huu kuwa mwafaka wa kuingia katika umiliki wa nyumba. Pata mkopo wa nyumba kwa kiwango cha riba kisichobadilika kutoka KMRC na uanze kubadilisha malipo yako ya kodi kuwa nyumba yako.
2. Panga safari yako kwa bidii.
Huna haja ya kuwa milionea ili kumiliki boma - mpango mzuri utatosha. Kila malipo ya kodi ni pesa ambayo hautawahi kuona tena. Kwa nini usigeuze malipo hayo kuwa uwekezaji katika maisha yako ya baadaye? Kupanga mikakati ya safari yako kutakuruhusu kutumia rasilimali zako kikamilifu na kupunguza vikwazo.
3. Imarisha ujuzi wako wa kifedha
Maarifa ndiyo tiba ya woga na imani potofu zote zinazoweza kukurudisha nyuma. Tenga muda kuelewa dhana za kifedha kama vile viwango vya riba visivyobadilika dhidi ya vinavyobadilika, gharama za matukio na hata kodi. Ujuzi huu utakusaidia kujenga mikakati thabiti na kukulinda kutokana na hatari. Unaweza kufikia nyenzo za elimu za KMRC kwenye tovuti yake na kurasa za mitandao ya kijamii.
4. Elewa soko la nyumba.
Mambo kama vile ugavi na mahitaji, mfumuko wa bei na sera za serikali yote huathiri bei ya nyumba. Kuelewa mambo haya kutakuruhusu kufanya maamuzi sahihi kuhusu wakati mwafaka wa kuchukua mkopo wa nyumba na aina ya nyumba ya kuchagua.
5. Fikiria zaidi ya ununuzi
Kuwa mmiliki wa nyumba ni uamuzi mkubwa ambao unaweza kukufaidi kwa miaka mingi. Zingatia matarajio ya siku zijazo kama vile kubadilisha taaluma, kuanzisha familia, kustaafu na malengo mengine ya kibinafsi unapochagua nyumba ya ndoto zako. Hii itakuwezesha kufanya chaguo linalostahili na linalofaa, kufungua uwezekano usio na mwisho.
Tunaweza kujumlisha yote kwa mambo matatu - kufanya kazi na
taasisi sahihi ya kifedha, kujiwezesha na maarifa na kupanga mikakati ya
mafanikio. KMRC wanadhamira nyumba za bei nafuu kufikia Wakenya wote.
Tembelea tovuti yao www.kmrc.co.ke ili kujifunza zaidi kuwahusu na jinsi ya kupata
rasilimali zao.