logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shabiki wa Arsenal auawa baada ya kutofautiana kuhusu mechi ya Man united na Arsenal

Mwili wa mwathiriwa ulipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kabwohe kwa uchunguzi wa maiti

image
na Radio Jambo

Habari05 September 2023 - 12:32

Muhtasari


  • Kulingana na Tumusiime, mshukiwa huyo kwa sasa anafuatiliwa na polisi baada ya mwathiriwa anayedaiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani kufariki.
mashabiki wa Arsenal.

Kijana wa miaka 22 kutoka Wilaya ya Sheema nchini Uganda anadaiwa kumuua shabiki wa Arsenal kufuatia kutofautiana kuhusu mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Arsenal na Man United siku ya Jumapili.

Kulingana na Citizen Digital Kwa mujibu wa polisi, Jackson Aineruhanga aliuawa muda mfupi baada ya ushindi wa Arsenal dhidi ya Man United.

Wapenzi hao wawili wa kandanda walizozana baada ya bao la mchezaji wa Manchester United Alejandro Garnacho kufutwa kwa sababu ya kuotea.

“Inadaiwa jioni baada ya mechi, washabiki hao wawili walizua kutoelewana walipokuwa wakitazama mechi. Wawili hao baadaye walienda kwenye baa na wakafukuzwa kwa kusababisha fujo, na hapo ndipo vita vilipozidi,” msemaji wa Polisi Marcial Tumusiime alisema akinukuliwa na gazeti la Monitor.

Kulingana na Tumusiime, mshukiwa huyo kwa sasa anafuatiliwa na polisi baada ya mwathiriwa anayedaiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani kufariki.

Tumusiime anabainisha kuwa kuna uchunguzi unaendelea na sampuli zimekusanywa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

"Tulitembelea eneo la uhalifu na kukuta kipande cha fimbo kikiwa na madoa ya damu na viatu vya washukiwa," alisema.

Mwili wa mwathiriwa ulipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kabwohe kwa uchunguzi wa maiti

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved