Bungoma: Gavana awajibu Gen-Z kuhusu 'matumizi ya Sh25m kwa maua' sikukuu ya Madaraka

‘Pesa za sikukuu ya Madaraka: Eleza matumizi ya sh148m haswa sh25m zilizotumika kwa maua, sh15m zilizotumika kwenye mikutano na matumizi mengine husika.’ moja ya maswali yalisoma.

Muhtasari

‘Pesa za sikukuu ya Madaraka: Eleza matumizi ya sh148m haswa sh25m zilizotumika kwa maua, sh15m zilizotumika kwenye mikutano na matumizi mengine husika.’ lilisoma swali .

GAVANA KEN LUSAKA.
GAVANA KEN LUSAKA.

Gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka hatimaye amenywea kwenye shinikizo la vuguvugu la Gen Z kuwajibisha viongozi katka kila kaunti na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha za kaunti hiyo.

Kaitka kikao chake na waandishi wa habari, gavana Lusaka amelazimika kunyoosha maelezo kuhusu kile vijana wa Gen Z walidai Sh25m zilitumiwa katika ununuzi wa maua wakati wa sherehe za sikukuu ya Madaraka Juni mosi.

Vijana hao walikuwa wamemuandikia gavana Lusaka barua wakitaka kujua jinsi fedha hizo zilitumiwa.

“Mnamo Jumanne Julai ya tarehe 16, 2024, vijana wa Bungoma waliwasilisha ombi katika ofisi yangu kuhusu masuala kadhaa ambayo yalihitaji majibu yangu. Nimepitia maombi yao na ningependa kuyajibu kama ifuatavyo,” Gavana Lusaka alianza.

‘Pesa za sikukuu ya Madaraka: Eleza matumizi ya sh148m haswa sh25m zilizotumika kwa maua, sh15m zilizotumika kwenye mikutano na matumizi mengine husika.’ moja ya maswali yalisoma.

“Jibu langu ni kwamba pesa hizo zilipitishwa na bunge la kaunti ya Bungoma na kutumika kama ifuatavyo; elimu na mafunzo ya ufundi stadi sh 1m, mgao wa dharura sh1m, barabara na miundombinu ya umma sh24.8m, miundombinu mingine na kazi za kiraia na kuweka alama kwenye barabara sh6.8m, mabango na alama za tahadhari sh18m, biashara, nishati na viwanda sh13m, bili za umeme sh13m, ardhi mipango miji na kimwili sh25m, kurembesha miji sh25m, jinsia na utamaduni sh5m, maandalizi ya kitabu cha kaunti sh5m, vijana na michezo sh60m – hiyo ilikuwa kumaliza ujenzi wa awamu ya kwanza ya uwanja wa Masinde Muliro, usimamizi wa utumishi wa umma sh12m, huduma za upishi na vingine sh4m…” Gavana huyo aliendelea kudadavua mahesabu.

Matumizi mengine ambayo alielezea ni kwenye video hii hapa;