logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Alhamisi

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nakuru, Kiambu, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Siaya, na Mombasa.

image
na SAMUEL MAINA

Habari01 August 2024 - 04:44

Muhtasari


  • •Kampuni hiyo imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nakuru, Kiambu, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Siaya, na Mombasa.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 25. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nakuru, Kiambu, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Siaya, na Mombasa.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya Gitaru na Regen zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ngata, Ogilgei, na Piave katika kaunti ya Nakuru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Nyankoba na Birongo katika kaunti ya Nyamira pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Kisii, eneo la kiwanda cha chai cha Eberege litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Eneo la Karima Mission School katika kaunti ya Nyeri litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Gitwe na Kona Mbaya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Nango, Wagusum, na Sirongo katika kaunti ya Siaya yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Shanzu katika kaunti ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved