KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 25.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Murang'a, Meru, Kiambu, Nyeri, Homa Bay, Kakamega, Uasin Gishu.
Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Ndula, Kolping, Gatuanyaga, Landless na mtaa wa Kisii yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Langas na Kisumu Ndogo katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Meteorological katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Katika kaunti ya Homa Bay, maeneo ya Kikubi na Nyandiwa yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Munyange, Miirini, Gituiga, Kiawarigi, na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Kiengu, Kinna, na Garbatulla katika kaunti ya Meru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Nyakianga na Kenya Njeru katika kaunti y Murang'a pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.