KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa stima leo, Jumapili

Baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kisumu, Lamu, na Kisii.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Agosti 25.  

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kisumu, Lamu, na Kisii.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Babadogo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Pipeline Estate na Police Line katika kaunti ya Kisumu yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii pia zitakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa tisa alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Lamu na Mokowe katika kaunti ya Lamu zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.