Papa mwitu katika ufuo wa Brazili wamepatikana na chembechembe za cocaine, kulingana na utafiti mpya wa wanasayansi wa Brazili, katika utafiti wa hivi punde.
Kwa mujibu ripoti, utafiti huo unaonyesha jinsi matumizi haramu ya dawa za kulevya yanayofanywa na binadamu yanadhuru viumbe vya baharini.
Kulingana na utafiti wenye kichwa Cocaine Shark na kuchapishwa katika jarida la Science of the Total Environment, wanasayansi walichana miili ya papa 13 wenye ncha kali (Rhizoprionodon lalandii) walionaswa kwenye nyavu za wavuvi karibu na ufuo wa Rio de Janeiro.
Wote 13 walijaribiwa kuwa na dawa hiyo.
Tafiti za awali zimegundua kokeni katika maji ya mito, bahari na maji taka, na athari za dawa hiyo zimepatikana katika viumbe wengine wa baharini kama vile uduvi.
Utafiti tofauti hivi majuzi ulifichua kwamba viwango vya juu vya mabaki ya kokeini vilikuwa vikisababisha "athari kubwa za sumu" kwa wanyama kama vile kome wa kahawia, oysters na mikunga huko Santos Bay, katika jimbo la São Paulo la Brazili.
Lakini mkusanyiko uliopatikana katika papa wa Rio ulikuwa juu mara 100 kuliko ulivyopatikana katika wanyama wengine wa baharini, watafiti walisema.
Jinsi kokeini ilivyoishia kwenye papa bado ni kitendawili.
Kuna uwezekano kadhaa: moja ni kwamba dawa hiyo ilianguka baharini wakati wa usafirishaji au ilitupwa baharini na wasafirishaji haramu wakijaribu kukwepa mamlaka.
Brazili haizalishi kiasi kikubwa cha kokeini, lakini ni msafirishaji mkuu nje, huku magenge yenye nguvu ya mitaani kama vile First Capital Command (PCC) ikituma tani za dawa hiyo katika makontena ya usafirishaji hadi Ulaya, The Guardian waliripoti.