logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wahasiriwa wa ulipuaji wa ubalozi wa Marekani zaidi ya 300 wadai kufidiwa

Wahasiriwa wa ulipuaji wa ubalozi wa Marekani wameishtaki serikali ya Kenya kwa kukosa kuimarisha ulinzi kwenye mipaka na kuruhusu wanamgambo wa Al Qaeda kuingia nchini

image
na Radio Jambo

Habari18 May 2021 - 12:41

Muhtasari


•Wahasiriwa wameishtaki serikali ya Kenya kwa kukosa kuimarisha ulinzi kwenye mipaka na kuruhusu wanamgambo wa Al Qaeda kuingia nchini

• Wahasiriwa wamedai kuwa kufidiwa kwao kungeleta hisia ya kupona, haki na kuwa msaada mkubwa wanaouhitaji

ulipuzi wa ubalozi wa marekani1998

Zaidi ya wahasiriwa 300 wa ulipuzi wa mnara wa ubalozi wa Marekani mwakani 1998 wamekata rufaa wakidai kufidiwa na serikali.

Waathiriwa hao wameilamu nchi kwa kutojali maisha ya wananchi wake. Wamedai kuwa serikali haikuwa imeimarisha ulinzi kwenye mipaka na ndio maana wanamgambo wa Al Qaeda wakaweza kuingia nchini.

Tunaelewa kuwa kabla ya shambulizi lile, serikali ya Sudan iliwaficha wanamgambo wa Al Qaeda kwa kuwapa pasipoti za nchi hiyokisha kuwaruhusu kusafirisha silaha na pesa hadi Kenya” Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria, Dr Annete Mbogoh alisema kwenye hati ya kiapo aliyowasilisha kotini.

Waadhiriwa wale pamoja na Kituo cha sheria wamedai kuwa kufidiwa kwao kungeleta hisia ya kupona, haki na kuwa msaada mkubwa wanaouhitaji. Walileza kuwa waliendelea kukumbwa na shida za kisaikologia na kihisia.

“Maisha yetu yalipunguzwa kuwa maisha ya kutegemaeana na tunakumbana na vizuizi vingi ikiwemo kupoteza tuwapendao na machungu ya mauti “ Waadhiriwa hao walidai.

Waathiriwa wale wamelia kutengwa  na kusahaulika na serikali ya Kenya. Wanadai kuwa hakuna rekodi ya afisa yeyote ama taasisi yoyote iliyoadhibiwa kwa kuskosa kuzuia  tukio hilo licha ya kupewa ilani na serikali ya Amerika la kuhuzunisha

Kesi hiyo itatajwa tarehe ishirini na tano mwezini Mei.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved