logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afisa wa jela adaiwa kuibia kikundi watafuta kazi zaidi ya Sh200m

Sajini katika jela la wanawake la Lang'ata amekamatwa kwa kuwalaghai watafuta kazi wasiojiweza na kushiriki katika utengenezaji wa pesa bandia

image
na Radio Jambo

Yanayojiri22 May 2021 - 06:30

Muhtasari


•Mshukiwa pia alipatikana na dola bandia za kimarekani kiasi cha shilingi milioni 2.4

•Inadaiwa kuwa nasra alikuwa akiwaandikisha watafuta kazi wasiojiweza na kuwaitisha kiwango kikubwa cha pesa huku akiwaahidi kuwatafutia kazi katika mashirika ya serikali.

grace nyamohanga

Mwanamke mmoja ambaye ni sajini mkubwa katika jela ya wanawake ya Lang’ata kwa tuhuma za kuendesha biashara ya ulaghai.

Inadaiwa kuwa, Grace Nyamohanga almaarufu kama Nasra  ameibia kikundi cha watafuta kazi kisichotambulishwa zaidi ya milioni mia mbili kwa kipindi cha miezi kumi pekee. Grace pia anatuhumiwa kujihusisha na biashara ya kutengeneza pesa bandia baada ya kupatikana na Sh2.4m zikiwa katika mfumo wa dola ya kimarekani.

Kupitia akaunti ya Twitter, kurugenzi la DCI limeripoti kuwa Nasra amekuwa akiendesha shirika haramu ambalo huwaandikisha watafata kazi wasiojiweza huku ikiwaahindi kuwatafutia kazi katika mashirika makubwa ya kiserekali kama jeshi la Kenya (KDF) na idara ya polisi.

Kutokana na barua nyingi za kazi alizopatikana nazo, ilionekana kuwa mshukiwa huyo alikuwa amewaandikisha watafuta kazi kutaka makundi yote ya masomo.

Mwanamke mmoja toka Kiambu ni baina ya walioanguka kwenye mtego ule huku ikiripotiwa kuwa alipoteza Zaidi ya laki nane baada ya kuahidiwa kuwa watoto wake wangetafutiwa kazi katika shirika la NHIF, Huduma za mji mkuu wa Nairobi (NMS) na shirika la bandari za Kenya(KPA).

bandari la mombasa

Inadaiwa kuwa mwanamke yule alikuwa amepewa hadi barua za kuwaalika watoto wale kwenye mashirika yale ili kuchukua nafasi za kazi ambazo mshukiwa alikuwa amesema kuwa ni wazi. Hata hivyo, alianza kushuku uhalisi wa barua zile na ndipo akaripoti kesi hiyo kwa wapelelezi.

Mwezini Januari, mshukiwa alikuwa amefanya njama ya kuwaandikisha watafuta kazi sitini  waliopewa barua za kuwaalika kazi katika huduma ya wanja za ndege (KAA) huku wakilipa kati ya shilingi laki tatu na laki nne kila mmoja na hata kupelekwa kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na mtu aliyejifanya HR ili kujitambulisha na mahala watakapokuwa wanafanya kazi” DCI waliripoti.

Baadae watafuta kazi hao waliambiwa waende nyumbani na waripoti tarehe 18 mwezi wa Mechi ingawa hiyo ndio ilikuwa mara yao ya mwisho kuskia kutoka kwa wakora wale wakiongozwa na Nasra.

Uchunguzi zaidi umedhibitisha kuwa Nasra amekuwa akishirikiana na walinzi jela wengine kutekeleza biashara ile haramu ikiripotiwa kuwa kuna afisa mmoja alipokea Sh19m huku dereva akipokea Sh5.7m kwenye biashara hiyo.

"Kwa sasa, wapelelezi wanapeleleza zaidi ili kudhibitisha uhusiano wa mshukiwa na biashara ya kutengeneza pesa bandia baada ya dola za kimarekani kiwango cha Sh2.4 m kupatikana ndani ya makazi ya mshukiwa yaliyo kwenye makazi ya maafisa wa jela Industrial Area" DCI waliandika.

Wakenya waliokuwa wameanguka kwenye mtego huo wameagizwa kuandikisha ripoti kwenye ofisi kuu za DCI.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved