MCHAKATO WA BBI

Rais Kenyatta asema kuwa ana uhakika 'reggea' itafufuka

“Niko na uhakika kuwa yaliyo mbele yetu tutasuluhisha . Tukiwa na mawakili shupavu kama Orengo mnaona tukishindwa kweli?” Rais alisema.

Muhtasari

•Rais amesema kuwa mchakato huo ni wa kuhakikishia Wakenya maisha mema ya usoni

• Raila alihakikishia wakazi wa Nyanza kuwa mchakato wa BBI hauwezi kwama kwa namna yoyote huku akiagiza Rais kupeleka miradi zaidi upande huo wa Nyanza.

Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa anamini kuwa mchakato wa BBI utaweza kufufuliwa tena licha ya kizuizi kilichoikumba kwa sasa.

Rais pia amesema  kuwa mchakato huo ni wa kuhakikishia Wakenya maisha mema ya usoni huku akiwataka kukaa kwa amani kushirikiana kwa pamoja.

Akizungumza katika soko ya Wagai iliyo katika eneo bunge la Gem, kaunti ya Siaya, rais Uhuru alihakikishia wakazi kuwa ushirikiano wake na kinara wa ODM, Raila Odinga ni wa kudumu.

“BBI haisaidii Raila na familia yake, haisaidii Uhuru. Ni ya kuleta haki kwa Wakenya wote na ndio maana nawaomba mjitokeze kuunga mkono mchakato huu” Rais alisema.

Rais ambaye ako kwenye ziara upande wa Nyanza kabla ya kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya Madaraka yatakayofanyika katika uwanja mpya wa Kenyatta ulio kaunti ya Kisumu siku ya Jumanne alihimiza  wakazi  kuunga mkono mchakato wa BBI huku akileza imani yake kuwa maamuzi wa mahakama kuu dhidi ya BBI yatatupiliwa mbali.

“Niko na uhakika kuwa yaliyo mbele yetu tutasuluhisha . Tukiwa na mawakili shupavu kama Orengo mnaona tukishindwa kweli?” Rais alisema.

Kwa upande wake Raila aliambia wakazi kuwa mchakato wa BBI hauwezi kwama kwa namna yoyote huku akiagiza Rais kupeleka miradi zaidi upande huo wa Nyanza.

Rais alipongeza Raila kwa kusimama naye tangu salamu za ‘handshake’ mwakani 2018

“Tunawaagiza Wakenya kuhifadhi amani. Ndio maana namshukuru Baba kwani amesimama name tangu tusalimiane. Watu wanaichukulia virahisi na tunajua vizuri kinachofanyika watu wakigombana. Tulisema tutamaliza kumwagika kwa damu na tukasema kuwa Wakenya wanakuja mbele” Rais alisema.