logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mvulana mwenye umri wa miaka 17 amuua binamu yake kwa ugomvi wa kuchaji simu

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao walizozana kuhusu ni nani angechaji simu yake wa  kwanza

image
na Radio Jambo

Yanayojiri11 July 2022 - 07:54

Muhtasari


•Polisi katika eneo la Kaimosi kaunti ya Nandi wameanzisha msako wa kumsaka mshukiwa mwenye umri wa miaka 17 ambaye anadaiwa kumuua binamu yake siku ya Jumapili baada ya kutofautiana kwa sababu ya kuchaji simu ya rununu.

•Marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Josphat Kibet, 31, alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kapsabet, ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

 

Polisi katika eneo la Kaimosi kaunti ya Nandi wameanzisha msako wa kumsaka mshukiwa mwenye umri wa miaka 17 ambaye anadaiwa kumuua binamu yake siku ya Jumapili baada ya kutofautiana kwa sababu ya kuchaji simu ya rununu.

Kulingana na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wawili hao waligombana vikali kuhusu nani angeanza kuchaji simu yake wa kwanza.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao walizozana kuhusu ni nani angechaji simu yake wa  kwanza, kabla ya kijana huyo kuchukua mshale, na kumdunga marehemu upande wa kushoto wa kifua chake kabla ya kuondoka,” alisema DCI.

Marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Josphat Kibet, 31, alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kapsabet, ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Kwingineko ni kwamba, Polisi huko Webuye wamewakamata wanaume wawili kwa madai ya kuwaua jamaa zao kwa madai ya deni la Sh50.

Bw Nickson Matumbai, 61, alidaiwa kuuawa kwa kudungwa kisu na kakake mwenye umri wa miaka 33 na binamu yake mwenye umri wa miaka 50 katika lokesheni ya Misikhu katika Kaunti ya Bungoma mnamo Ijumaa.

Wawili hao wanashukiwa kutumia vitu  na kisu kumuua Bw Matumbai walipokuwa wakirejea nyumbani kutoka kwa ulevi kwenye pango la pombe haramu ya kienyeji. Inasemekana Bw Matumbai na mdogo wake walizozana kuhusu deni hilo la Sh50.

"Ni kweli ndugu zangu walikuwa wakipigana wakiwa wamelewa. Ninashuku kwamba binamu yangu pia anahusika (katika mauaji) na labda anajua ni nani mwingine aliyesaidia katika mauaji ya Matumbai," alisema mdogo wa marehemu James Makenzi.

Mwili wa Matumbai ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kaunti ya Webuye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved