logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afisa wa polisi auawa na gari lililokuwa kwa kasi Ruiru

Gari hilo halikusimama baada ya tukio hilo la saa nne usiku, polisi walisema.

image
na Davis Ojiambo

Habari14 May 2024 - 05:41

Muhtasari


  • • Mwathiriwa alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Ruiru na alikuwa akishika doria ajali hiyo ilipotokea.
  • • Waliyoshuhudia walisema kuwa marehemu alipata majeraha ya kichwa na kuvunjika mguu wa kushoto.
  • • Polisi walisema msako wa kumtafuta dereva aliyehusika na tukio hilo unaendelea.
Ajali

Afisa wa polisi aliuawa Jumatatu usiku katika ajali kwenye barabara ya Kiambu-Ruiru, kaunti ya Kiambu.

Afisa huyo alikuwa na mwenzake walipokuwa wakivuka barabara wakati aligongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.

Gari hilo halikusimama baada ya tukio hilo la saa nne usiku, polisi walisema.

Mwathiriwa alikuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Ruiru na alikuwa akishika doria ajali hiyo ilipotokea.

Mwenzake alikuwa na aliponea kwani alisita kuvuka baada ya kuona gari hilo likienda kwa kasi mno.

Waliyoshuhudia walisema kuwa marehemu alipata majeraha ya kichwa na kuvunjika mguu wa kushoto.

Alitangazwa kufariki alipofika katika hospitali ya Plainsview mtaani Ruiru.

Polisi walisema msako wa kumtafuta dereva aliyehusika na tukio hilo unaendelea.

Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved