Ni rasmi sasa msomi profesa wa sheria, KIthure Kindiki ndiye naibu rais wa 3 wa Kenya chini ya katriba mpya ya 2010 baada ya kula viapo katika ukumbi wa KICC Ijumaa asubuhi.
Aliapishwa siku ya Ijumaa kufuatia kuondolewa kwa maagizo ambayo yalikuwa yamechelewesha shughuli hiyo kwa takriban wiki mbili.
“Mimi, Kithure Kindiki, naapa kwamba nitatumikia kwa dhati na kwa bidii watu wa Kenya na Jamhuri ya Kenya katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya, kwamba nitatekeleza wajibu wangu kwa bidii na kutekeleza majukumu yangu katika afisi iliyotajwa kwa kadiri ya uamuzi wangu, kwamba wakati wote inapohitajika hivyo kwa uaminifu na kweli nitatoa baraza langu na kumshauri Rais wa Jamhuri ya Kenya, kwamba nitatenda haki kwa wote bila woga, upendeleo, mapenzi au nia mbaya na kwamba sitafichua moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja mambo ambayo yatanijia katika utupaji wa rangi zangu na kujitolea kwa usiri wangu, kwa hivyo nisaidie Mungu," Kindiki aliapa.
Alipokelewa kwa shangwe huku akisimama kula kiapo chake Anamrithi aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye alitimuliwa.
Kabla ya kuteuliwa na Rais William Ruto, Kindiki aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa. Baadaye alithibitishwa na Bunge.
Benchi la majaji watatu katika Mahakama Kuu liliondoa amri zilizokuwa zimezuia kiapo cha Kindiki siku ya Alhamisi.
Kindiki alifika katika ukumbi wa kuapishwa, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) saa 10 asubuhi akiandamana na mkewe Dkt Joyce Kindiki.