Jaji mkuu na rais wa mahakama ya juu zaidi Matha Koome amemwandikia barua waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen akiteta kuhusiana na swala la kunyang'anywa walinzi.
Barua sawia pia imemfikia mkuu wa polisi Douglas Kanja, akiwataka wawili hao kueleza kwa kina mbona walinzi wake waliondolewa.
Koome kwenye barua iliyofikia vyombo vya habari ametaja jambo hilo kama kuhitilafiana na kukandamiza uhuru wa mahakama.
Kwenye barua amesisitiza kwamba wanafaa kurejeshwa kwa haraka bila pingamizi.
Ametaja hilo kama njia moja wa kuwatia uwoga majaji hasa wanapotoa uwamuzi kwenye kesi zinazowahusisha maafisa walioko serikalini.
Hivi majuzi hakimu Lawrence Mugambi alimhukumu Inspekta mkuu wa polisi kifungo cha miezi sita gerezani kutokana na kosa la kudharau mahakama katika kesi iliohusisha ndugu wawili na mwanaharakati na huenda hili limechangia katika swala hilo la kuondolewa walinzi.
Matha Koome ameitaka idara ya polisi kuwarejesha walinzi wa Jaji Mugambi na ametaja hili kama kuhitilafiana na Uhuru wa mahakama.
"Mahakama imeshitushwa na jambo la kuondolewa walinzi wa Majaji, tunaomba kwamba walinzi warejeshwekulingana kulingana na katiba ili majaji na uhuru wac kufanya kazi yao kwa njia ya uhuru na haki," alisema Mata Koome.
Tunachukua nafasi hii kuwahakikishia wakenya kwamba mahakama itasimama thabiti katika kulinda ukweli na mwongozo wa sheria. Tunalaani vikali kitendo hicho na nawawataka mahakimu pamoja na idara ya usalama kuendelea kufanya kazi yao bila uwoga wowte.
Changamoto pia inazidi kuiandama mahakama, siku kadhaa zilizopita aliyekuwa Rais wa LSK Nelson Havi aliwasilisha kesi mahakamani akiwataka majaji wote nane wa mahakama ya juu zaidi nchini kujiuzulu.