Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa sasa anasema kwamba wakati watamtaka Gachagua watamurejesha.
Didimus alizungumza Jumapili akieleza kwamba kuna wakati utafika na watamuhitaji Gachagua katika serikali ili kufanikisha malengo yao.
Alieleza kwamba Gachagua hakuwa mbaya ila kushikilia ofisi ya naibu wa Rais wa kenya ndio haikumfaa.
Baraza pia ameondoa hofu kwamba wapinzani wao wameanza kujipanga akisema yote wapinzani wamefanya watahitaji mikutano miwili tu kusambaratisha juhudi zao zote.
" Hawa adui zetu, wapinzani wetu ni kazi rahisi sana, mikutano miwili pekee itaweza kusambaratisha yote ambayo wamepanga. wakati wa kampeni ukifika, wakati mwingine siasa sio kuhusu watu ambao unapenda, ni kuhusu watu unahitaji na unawataka wakati huo".
"Wakati ukifika hata yule Rigathi ambaye tulimung'oa mamlaka iwapo tutamuhitaji tutamurejesha. Hakua tu mzuri kufanya kazi kama Naibu wa rais wa Kenya lakini bado anaeza kuwa mzuri kuwa mpiga kura au kuwa mwanachama wa muungano wetu". alieleza Didmus
Didimus alisistiza kwamba walimueka Gachagua nje ya serikali ili kupata funzo kwamba alikuwa naibu wa rais wa Kenya ila si watu wa mlima Kenya pekee.
"Nina imani kwamba sasa Gachagua amejifunza na anaelewa kwamba ukikua naibu wa rais unakuwa mtu ambaye unapenda makabila yote" aliendelea kueleza mbunge Didimus
Mbunge huyo pia ameelezea imani yake kwamba kabla ya uchguzi ujao wa 2027 watakua wamefaulu kumurejesha Gachagua na kumukaribisha tena kuwa mwanachama wa UDA na apewe kazi ingine yenye anaezaifanya.
"Tuna imani kwamba kabla ya 2027 mwezi wa tano atakua amebadilika na tutamrejesha kama mwanachama wa UDA akae hapo kama mwanachama na tumutafutie kazi ingine yenye anaezafanya wakati huo ukifika kwa hivyo msiwe na shaka." alisema Didimus Barasa.