
Aliyekuwa naibu wa rais wa zamani Rigathi Gachagua kwa mara ya kwanza amezungumzia wazi kuhusu kubanduliwa kwake madarakani kama naibu wa rais.
Akizungumza wakati wa mahojiano ya moja kwa moja siku ya Jumanne (Februari 4,2025) Gachagua alisema kuwa hana nia yoyote ya kuwania kiti chochote cha uongozi nchini akishikilia usemi kuwa si lazima ashikilie kiti cha uongozi nchini kwani haina maana kwa sasa kwake.
Naibu huyo wa zamani amedokeza kuwa wakati wa kung'atuliwa kwake uongozini alishawishiwa na rais pamoja na wandani wa rais ili ajiuzulu ndio apate nafasi ya kuwania kiti cha urais tena.
''Mambo ya eti nikifukuzwa sitasimama tena hiyo haina maana kwangu unajua watu wanafikiria mimi ni mtu wa kujipenda sana.Sio lazima nikuwe chochote katika hii Jamhuri ya kenya . Na mimi kama ningesikiliza vile rais alikuwa ameniambia nijiuzulu kwa vile alikuwa ameniambia nikupee bilioni mbili.uwende nyumbani uwende upumzike ufanye mambo yako ukue na security ukuwe na mshahara na unaweza simama siku nyingine.''
''Sasa nikajiuliza yule anakupangia mabaya anaweza kukupangia vile utaishi hata wabunge wanaoniunga mkono walikuja kuniambia wewe jiuzulu ndio upate nafasi ya kusimama nikasema hiyo ni kujipenda sio lazima mimi nisimame ama lazima mimi niongoze mimi lazima nijitolee nitetee Wakenya na ukweli ujulikanne Gachagua akasema'
Kwa kuongezea Gachagua alisema ikiwa angetaka kuwania kiti chochote cha siasa bado anaweza kusimama kwa sababau angali ana kesi ambayo inaendelea mahakamani akasema kuwa sheria ya Kenya iko wazi unaweza wania kiti hata kama ungali una kesi inayoendelea akitoa mfano wa aliyekua rais wa zamani Uhuru Kenyatta na William Ruto walipowania kiti cha urais ilihali walikuwa na kesi iliyokuwa imewaandama.
Alipuzilia mbali juhudi zake za kutaka kusimama akisema kuwa kwa sasa analenga kuhakikisha kuwa wakenya wanaishi vizuri ''Sio lazima ati mimi ndio nikuwe kiongozi wa Kenya iko watu wengi wakuongoza mimi nitakuwa kwa ile timu ya kupanga lakini hamna mtu amenikataza kusimama mimi niko na kesi kortini inaendelea.
''Uhuru na Ruto walisimama wakiwa na kesi kwa Hague katiba ya Kenya iko wazi ya kwamba kama ungali na kesi kortini right yako ya kuwania kiti hauwezi ondolewa.Kwa hivyo mimi nikitaka kiti au kusimama nitasimama lakini hiyo haina haja ,saa hii ile kitu ya maana ni vile tutapanga hii Kenya na wengine ndio tuweze kupata uongozi bora''.
Gachagua alisema kuwa yeye si kiongozi wa mlima Kenya ila anafanya tu juhudi za kushirikiana na viongozi kutoka upinzani ili kujenga taifa bora tena lenye maono mazuri.''mimi ni mwananchi wa kawaida na niko na wafuasi wengi sana ambao wananiamini wananitegemea na ninaendelea kutafuta mbinu na njia vile hii Kenya itaendelea vizuri na nitachangia kiasi fulani kupanga hii kenya na kutafuta uongozi bora na ndio maana nimeanza kushikana na viongozi wengine katika Jamhuri ya Kenya tukiwa na mikakati ya kukubaliana vile hii Kenya itakaa na sio eti mimi ni kiongozi wa upinzani mimi ni kiongozi wa kusema ukweli''. alisema bwana Gachagua.