
Spika wa bunge la taifa Moses Masika Wetang'ula alikabiliwa
na hali tete kisheria kufuatia uamuzi wake wa kutotii agizo la mahakama.
Kutokana na tangazo lililotolewa mnamo Februari 12,2025 mahakama
ilitoa uamuzi na kusema kuwa muungano wa Azimio ulikuwa na idadi kubwa ya
wabunge kushinda muungano wa Kenya Kwanza.
Mahakama ilitoa agizo hilo ikisesema kuwa ni kinyume cha Spika
Wetang'ula kushikilia wadhifa huo kama spika wa bunge la taifa akiwa pia ndiye kiongozi
wa Chama cha Ford Kenya wakati ambapo yeye pia ni mwanachama wa muungano wa
kenya kwanza na vilevile mwanachama wa baraza la muungano wa Kenya kwanza.
Kutokana na hayo yote korti ilibaini kuwa ulikuwa ni ubatili
na kinyume cha sheria hivyo ikatoa uamuzi wa spika kufanya mabadiliko ya
kisheria na kuzingatia Katiba.
Wakati ambapo vikao vilirejelewa bungeni baada ya likizo
fupi spika aligairi kuzingatia maagizo
ya mahakama na kuutangaza muungano wa Kenya kwanza kuwa ndio uliokuwa na idadi
kubwa ya wabunge .
Kutokana na hilo la spika kutotii maamuzi ya mahakama
walalamishi zaidi ya 12 walifika katika mahakama ya rufaa wakitaka mahakama
hiyo kumshurutisha spika kutiii agizo la mahakama kuu na kuzingatia uamuzi
uliotolewa na jopo la majaji watatu.
Walalalmishi hao wakiongozwa na Kennedy njagi,Suba chachi na
Amos Wanjala walifika katika mahakama hio ya rufaa wakiwa na ombi la kurai
mahakama iweze kubatilisha tangazo jipya la Spika la kutangaza tena muungano wa
Kenya Kwanza kama waliowengi.
Kesi hio inajiri wakati ambapo mageuzi mbalimbali yanatarajiwa
kufanywa katika kamati mbalimbali za mabunge yote mawili bunge la taifa na lile
la seneti
Kulingana na maaumuzi ya spika Wetang'ula alisema kuwa katika
maamuzi ya mahakama haikutoa maelezo zaidi ya ni nini kifanyike hivyo kuliacha
bunge la taifa katika hali ngumu ya kutekeleza maamuzi hayo hivyo kusema kuwa
maamuzi yote yalitolewa na bunge la taifa kwa sababu ni taasisi huru hivyo ilitekeleza
maamuzi yake pasi kuingiliwa wala kuegemea
upande wowowte.