logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waandamanaji wateketeza kituo cha polisi cha Shauri Moyo Nairobi

Mvulana HUYO mwenye umri wa miaka 17 anasemekana kuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu.

image
na Davis Ojiambo

Yanayojiri05 March 2025 - 12:14

Muhtasari


  • Kulingana na kamanda wa polisi wa Nairobi George Sedah, kulikuwa na visa vya uhalifu katika maandamano hayo na mali kuteketezwa.
  • Polisi walikuwa wamesimamisha kundi la vijana kwa ajili ya msako kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.

Kituo cha polisi cha Shauri Moyo jijini Nairobi kimeteketezwa moto na kundi la vijana wenye hamaki wakidai majibu kuhusu kuuawa kwa kwa mvulana wa miaka 17 baada ya kupigwa risasi.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 17 anasemekana kuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Machafuko hayo yaliyoanza Jumatano asubuhi, pia yalishuhudia magari mawili ya polisi yakiteketezwa na mioto kuashwa barabarani.

Polisi walifyatua vitoa machozi kutawanya kundi la vijana katika eneo hilo kwa nia ya kutuliza hali.

Kulingana na kamanda wa polisi wa Nairobi George Sedah, kulikuwa na visa vya uhalifu katika maandamano hayo na mali kuteketezwa.

Alisema maandamano hayo yalitokana na tukio la Jumanne usiku ambapo ufyatulianaji wa risasi ulitokea eneo la Majengo Social Hall ukihusisha askari polisi ambao walikuwa wamevalia raia na kundi la vijana.

Polisi walikuwa wamesimamisha kundi la vijana kwa ajili ya msako kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.

Walikuwa wakimlenga mshukiwa maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa kundi hilo.

Katika hali hiyo, mshukiwa alikaidi amri na kupiga mayoye akiomba msaada kutoka kwa kundi lililokuwa likitoka msikitini.

Polisi walisema kundi hilo liliwashambulia na kuwakimbiza maafisa hao, na kumlazimu mmoja wao kufyatua risasi ili kujiokoa.

Hapo ndipo mtu mmoja alipopigwa risasi na kujeruhiwa kichwani na kufariki akikimbizwa hospitalini.

Polisi walisema mmoja wa maafisa wa polisi waliohusika katika makabiliano hayo alikuwa na majeraha mabaya kwenye nyonga, mkono na mgongoni.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved