logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshtuko huku jamaa akifungua na kuendesha kituo chake cha polisi Kesses bila mamlaka kujua

Ugunduzi huo ulifanyika Jumamosi baada ya maafisa wakuu wa polisi wa eneo hilo kutembelea kituo hicho.

image
na CYRUS OMBATIjournalist

Yanayojiri09 March 2025 - 14:29

Muhtasari


  • Mshukiwa alianzisha kituo cha doria ya polisi ndani ya mtaa wa Cherus, katika moja ya majengo ya mwenye nyumba, kwa kukipaka rangi za jeshi la polisi.
  •  Alifanya hivyo bila ufahamu wa maafisa wakuu wa polisi, hali iliyosababisha uchunguzi wa kina kufanyika.

Kituo haramu cha polisi kilichoanzishwa na mshukiwa.

Mwanaume mmoja alifungua na kuendesha kituo cha polisi katika eneo la Cheboror, Kesses, Uasin Gishu, bila mamlaka za polisi kufahamu.

 Ugunduzi huo ulifanyika Jumamosi baada ya maafisa wakuu wa polisi wa eneo hilo kutembelea kituo hicho.

 Ilikuwa mshtuko kwa maafisa wakuu wengi, waliodai maelezo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.

 Haijabainika kwa muda gani mtuhumiwa aliendesha kituo hicho cha polisi.

 Polisi walisema waligundua kuwa kituo hicho kilikuwa kinafanya kazi bila idhini ya mamlaka mnamo Machi 8 saa tano asubuhi.

Mtuhumiwa ni mkazi wa kijiji cha Asis, eneo la Ndugulu, tarafa ya Kesses, kaunti ya Uasin Gishu.

 Alifanya uamuzi wa kuanzisha kituo cha doria ya polisi ndani ya mtaa wa Cherus, katika moja ya majengo ya mwenye nyumba, kwa kukipaka rangi za jeshi la polisi.

 Alifanya hivyo bila ufahamu wa maafisa wakuu wa polisi, hali iliyosababisha uchunguzi wa kina kufanyika.

 Polisi wamesema wanaendelea kuchunguza suala hilo.

 Wanataka kujua kwa muda gani mwanamume huyo aliendesha kituo hicho na iwapo baadhi ya maafisa wa polisi walifahamu kuhusu uwepo wake.

 Wakazi watahojiwa ili kubaini kama waliwahi kukamatwa na kupelekwa katika kituo hicho.

 Vituo kama hivyo hupitia mchakato wa kisheria na kiserikali kabla ya kuzinduliwa na kuanza kufanya kazi rasmi.

 Vituo hivyo vinapaswa kuwa na silaha, selo, ofisi, na vyoo vinavyofanya kazi ipasavyo.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved