logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waziri Justin Muturi asisitiza kwamba hawezi kung'atuka ofisini kwa kusema ukweli

Waziri wa utumishi wa umaa Justine Muturi amesisitiza kwamba kamwe hatajiuzulu kutoka ofisini kwani hana kosa alilolifanya.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri20 March 2025 - 14:42

Muhtasari


  • Muturi pia amefichua kwamba tayari amemwandikia rais barua akitaka majibu kuhusu ni nani anaendeleza utekaji nyara na mauwaji ya kiholela.
  • Kwenywe waathiriwa wa utekaji nyara alikuwemo mwanawe waziri huyo wa utumishi wa umaa Lesley Muturi, jambo ambalo huenda limemchochea waziri huyo kupinga jambo hilo hadharani.
Public Service Cabinet Secretary Justin Muturi
Waziri wa utumishi wa umaa Justin Muturi amesisitiza kwamba kamwe hatajiuzulu kutoka ofisini kwani hana kosa alilolifanya. Muturi ameshikilia kwamba hawezi kujiondoa ofisini kwa kusema ukweli uilopo akieleza kwamba hakuna mkenya asiyefahamu kuhusu utekaji nyara ambao unaendelea nchini. 

Waziri huyo akizungumza katika kaunti ya Mombasa akiongoza kufungwa kwa kongamoano la mataifa barani Afrika amefichua kwamba tayari amemwandikia rais barua akitaka majibu kuhusu ni nani anaendeleza utekaji nyara na mauwaji ya kiholela.

Muturi amemtaka Rais William Ruto kujitokeza wazi na kuelezea wakenya ni nani aneyeendeleza dhuluma za utekaji nyara na mauwaji kwa watu wasio na hatia. Ameongeza kwamba anasubiri majibu kutoka kwa rais.

"Tumesema kama serikali kwamba hatuungi mkono jambo la utekaji nyara na pia mateso ya watu kuuliwa hapa nchini. Sasa yule mtu ambaye anakashifu jambo hilo, ni yeye anafaa kutoka ama mimi. Yule ambaye ananiambia nitoke basi anasema anaunga mkono utekaji nyara na kuuliwa kwa watu kiholela, kinyume cha sheria," aliweka wazi waziri huyo.

"Nani hapa anatakiwa kuwajibika? Lile jambo la kusema utoke ujiiuzulu, utajiuzulu kwa kusema ukweli? Ama kwa nini? Lazima mtu aseme ukweli wake pale. Na kama kuna makosa niko tayari kuyatetea vilivyo hata kama nitakuwa upande gani," alisisitiza.

Waziri huyo wa utumishi wa umaa amekuwa kipaumbele kupinga hadharani kuzembea kwa serikali hasa kuhusu swala la utekaji nyara kwa wakenya hasa vijana wa umri wa makamo.

Maswala ya utekaji nyara yaliana hapa nchini siku chache tu baada ya maandamono ya vijana wa Gen-Z kukamilika mwishoni mwa mwaka jana.

Kwenywe waathiriwa wa utekaji nyara alikuwemo mwanawe waziri huyo wa utumishi wa umaa Lesley Muturi, jambo ambalo huenda limemchochea waziri huyo kupinga jambo hilo hadharani licha ya kuwa kwenye srikali husika.

Waziri Muturi hii ni mara yake ya tatu akizungumza hadharani kwenye vyombo vya habari akimtaka rais Williamu Ruto kuelezea wazi kuhusu wahusika wa utekaji nyara na kukomesha mara moja.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved