logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Natembeya akashifu kushambuliwa kwa Mbunge Peter Salasya katika uwanja wa Nyayo

Natembeya alikashifu vikali tukio lililotokea jana la Mbunge Peter Salasya kushambuliwa.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri24 March 2025 - 15:12

Muhtasari


  • Natembeya aliweza kulaani tukio hilo akisema kuwa ni kitendo cha aibu ambacho hakifai kuvumiliwa na akasisitiza kuwa ni vyema kuwe na hali ya ubinadamu katika kila hali ili kuwezesha umoja wa kitaifa na Aamani.
  • Natembeya aliweza kusema kuwa kwa kuangazia tukio lililofanyika kule Nyayo linarudisha chini juhudi zilizopigwa nchini za kujenga demokrasia komavu na endelevu ambayo ina usawa kwa wote.

Gavana wa Trans Nzoia  George Natembeya alikashifu  vikali tukio lililotokea siku ya Jumapili la Mbunge Peter Salasya kushambuliwa na vijana ugani Nyayo.

Natembeya aliweza kulaani tukio hilo akisema kuwa ni kitendo cha aibu ambacho hakifai kuvumiliwa na akasisitiza kuwa ni vyema kuwe na hali ya ubinadamu katika kila hali ili kuwezesha umoja wa kitaifa na amani.

Katika mtandao wake wa X, Natembeya aliweza kusema kuwa kwa kuangazia tukio lililofanyika kule Nyayo linarudisha chini juhudi zilizopigwa nchini za kujenga demokrasia komavu na endelevu ambayo ina usawa kwa wote.

''Ninalaani tukio la Jana kwa mheshimiwa Mbunge wa Mumias Mashariki  Peter Salasya katika uga wa Nyayo alipofukuzwa na kushambuliwa na vijana wahuni,tukio hilo ni la unyama na ukiukaji mkubwa wa sheria, ''Natembeya alisema.

Alisisitiza kuwa katiba ya Kenya inaruhusu kila mmoja kuegemea katika mrengo wowote anaupenda na vilevile kuna uhuru wa kujieleza haki ambazo zinastahili kuheshimiwa na kila mmoja.

'' Tukio hili la kinyama linachochea uvunjaji mkubwa wa sheria kila mtu ana haki ya  kuunga au kupinga mrengo  wowote wa kisiasa au hata kuunga au kupinga sera ambazo yeye hakubaliani nazo kama taifa tunastahili kukashifu tukio hili ambalo linachochea usalama wa taifa au nchi''.

'' Tunastahili kupigania usawa, haki na masuala ambayo yanajenga uzalendo wetu kama taifa kuna masuala ambayo tunastahili kuwa tukipigania kama vile mijadala kuhusu hali za afya katika hospitali zetu,masuala ya maendeleo kwa  taifa bali si vurugu na kupinga viongozi walio na sera au misimamo  tofauti.

Viongozi wengine waliokashifu tukio la Peter Salasya kushambuliwa ni Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, mbunge wa Saboti Caleb Amisi ambao wote kwa kauli moja walilaani tukio hilo la kinyama.

Mudavadi alilisisitiza kuwa Demokrasia ya Kenya inaegemea kwa kuzungumza na heshima kwa wote pasi na upendeleo wowote.

''Kilichomtendekea mheshimiwa Peter Salasya katika uga wa Nyayo ni tukio la kusikitisha  na linashusha chini demokrasia ya taifa kwa vile watu wana uhuru wa kutangamana na kutoa maoni tofauti Mudavadi aliandika katika ukursa wake wa   X tarehe 23 Machi,2025.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved